TANZIA: Taarifa kuhusu vifo vya watumishi watano (5) wa Shirika la Reli Tanzania(TRC)

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
TAARIFA YA AJALI YA TRENI YA UOKOAJI NA KIBERENGE NAMBA HDT-3

Dar es Salaam, Machi 23, 2020.

Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC unasikitika kutangaza taarifa ya vifo vya watumishi wake
watano (5) kutokana na ajali ya treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge Na. HDT - 3 katika eneo lililopo kati ya Stesheni ya Mwakinyumbi na Gendagenda katika reli inayotoka Ruvu Junction mpaka Mruanzi Junction, tarehe 22 Machi 2020.

Ajali hiyo imehusisha watumishi sita (6) wa TRC ambapo watumishi wane (4) walifariki eneo la ajali na majeruhi wawili (2) walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya (Magunga) iliyopo Korogwe mkoani Tanga kwa ajili ya huduma za kitabibu, ilipofikia saa tano usiku (23:00) tarehe 22 Machi 2020 majeruhi mmoja (1) alifariki na kufikia jumla ya vifo vya watumishi watano (5) katika ajali hiyo.

Watumishi waliopoteza maisha katika ajali ni;
1. Ramadhani Gumbo – Meneja Usafirishaji Kanda ya Tanga
2. Eng. Fabiola Moshi – Meneja Ukarabati wa Mabehewa ya Abiria kanda ya Dar es Salaam
3. Joseph Komba – Meneja Msaidizi Usafirishaji Kanda ya Dar es Salaam
4. Philibert M. Kajuna – Mtaalamu wa Usalama wa Reli
5. George Urio - Dereva wa Kiberenge

Mpaka sasa majeruhi mmoja (1) Elizabeth Bona ambaye ni muongoza treni anaendelea na matibabu.
Aidha, uchunguzi wa kujumuisha kwa kushirikiana na taasisi nyingine utafanywa ili kubaini chanzo cha
ajali hii, uongozi unatoa pole kwa familia, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Shirika la Reli Tanzania kwa msiba huu pia taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kuhusu maandalizi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wetu.

Bwana ametwaa na Bwana ametoa, jina lake lihidimiwe.

Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC
TANZIA TRC.jpg


POLISI WAZUNGUMZIA AJALI YA WAFANYAKAZI WA TRC:

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonce Rwegasira amethibitisha kutokea kwa tukio la ajali ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkoa wa Tanga na kusababisha vifo vya watu watano katika Kitongoji cha Mgongola 'B' Tarafa ya Kabuku wilayani Handeni baada ya kiberenge walichokuwa wakisafiria kugongana na mabehewa ya treni.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospital ya Wilaya ya Korogwe huku majeruhi mmoja akiendelea kupatiwa matibabu katika hospital hiyo.
 

Attachments

  • TANZIA TRC.pdf
    492.1 KB · Views: 2
Tunasubiri taarifa ya uchunguzi, kwani tumezoea kusikia Bodaboda imegonga Treni au Mtembea kwa miguu amegonga Treni......
 
Back
Top Bottom