Tanzia: Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia

Jan 9, 2020
54
95
Mwandishi Nguli wa Kazi za Fasihi ya Kiswahili Prof. Euphrase Kezilahabi amefariki dunia. Tutamkumbuka Kezilahabi kwa kazi zake kama Rosa Mistika, Uwanja wa Fujo, Kaptula la Marx, Nagona na Mzingile! Alitetea Mashairi ya Kisasa!

Hakika, Jabali limeanguka! Tumeondokewa pakubwa.

Pumzika kwa amani Euphrase Vincent Mfunzi Bagaza Tilibuzya Kezilahabi😭😭

Soma; Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
IMG_20200109_220329_738.jpg

====
Huyu E. Kezihalabi ni nani?

Euphrase Kezilahabi alizaliwa 13 Aprili 1944 huko Namagondo kisiwani Ukerewe kilichopo ndani ya Ziwa Viktoria. Babake Vincent Tilibuzya alikuwa msimamizi wa kijiji na Euphrase alikuwa na ndugu 10 yaani wavulana 5 na wasichana 5. Alisoma shule ya msingi ya Nakasayenge halafu tangu 1957 Seminari ya kikatoliki ya Nyegezi aliyomaliza mwaka 1966.

1967 alijiandiskisha kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma ualimu na fasihi hadi digrii ya B.A. katika mwaka 1970. Mwaka uleule 1970 akawa mwalimu wa shule ya sekondari Mzumbe (Morogoro) halafu kwenye shule ya sekondari ya Mkwawa (Iringa).

1971 alirudi chuoni Dar es Salaam akawa mhadhiri msaidizi wa chuo alipoandika pia tasinifu ya M.A. kuhusu riwaya za Shaaban Robert, tangu 1974 mhadhiri kamili na 1978 mhadhiri mwandamizi. Akaendelea na masomo ya Ph.D. huko Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Wisconsin Madison alipotoa tasinifu yake mwaka 1985 kuhusu "African Philosophy and the Problem of Literary Interpretation". Sasa (mwaka 2012) ni profesa wa lugha za Kiafrika kwenye Chuo Kikuu cha Botswana.

Uandishi wake fikirishi uliowahi mletea shida sana kisiasa
kwa wale wenzangu ambao wamekuwa na utamaduni wa kujisomea bila shaka napotaja jina la Euprase Kezihalabi si geni masikioni mwao. Ukiacha ambao walisoma vitabu vyake wakiwa shule kwenye fasihi. binasfi nilianza kusoma vitabu vyake nikiwa nyumbani nikisoma kama burudani kabla ya kuja kufaham baadaye kile kilichokuwa kimeandikwa na athari zake. Nilisoma vitabu kama Rosa Mistika, Kichwa maji ,Dunia Uwanja wa Fujo,Gamba la Nyoka na Kaptula la Marx.

Vitabu hivi vitatu vilikuwa na ukakasi mwingi sana kufikia hatua viwili kati yake kufungiwa au kuzuiwa kuuzwa. Rosa Mistika na Kaptula la Max.

Zaidi Soma:
1. Kaptula la Marx: Unafahamu kwanini kitabu hiki kilipigwa marufuku? Waandishi wetu na Siasa zetu
 
RIP mtunzi wa Rosa Mistika
Namkumbuka sana kwa hicho kitabu Rosa mistika nilikisoms Kati ya mwaka 1976 na 1977

Sent using Jamii Forums mobile app
Rosa Mistika, nakumbuka kazi yake hii adhimu
Bado ninakumbuka kipande hiki cha simulizi zake R.i.P

Huko kisiwa cha Ukerewe kulikuwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Regina. Regina na jamaa yake waliishi pamoja katika kijiji cha Namagondo. Regina alikuwa mzuri sana lakini alikuwa na bwana
aliyemtesa. Regina alikuwa na binti watano; Rosa Mistika, Flora, Honorata, Stella, na Sperantia. Mume wa Regina aliitwa Zakaria na alitaka sana kupata mtoto wa kiume. Regina alikuwa na
mimba sasa na alimwomba Mungu ampe mtoto wa kiume.
Usiku mmoja, Regina alikuwa akila chakula cha jioni pamoja na watoto wake. Alizungumza nao juu ya mambo ya malezi. Baadaye walikwenda kulala. Wakati huo huo, Zakaria alikuwa akirudi kutoka mahali pa kunywa pombe. Alilewa sana na alimwambia Regina kwamba alitaka kuwaona watoto wake. Watoto waliitwa isipokuwa Rosa kwa sababu Rosa alikuwa ameanza kuwa mtu mzima. Zakaria aliwaambia waimbe na kufanya mazoezi ya kijeshi. Mara Stella alimwambia baba yake kwamba Rosa alipokea barua pamoja na pesa. Zakaria alikasirika. Hakutaka binti zake watembee na mvulana ye yote. Rosa aliitwa na Zakaria na aliulizwa juu ya barua hiyo.
Rosa hakumtaka babake asome barua yake. Alijaribu kuila, lakini Zakaria alimshika Rosa shingo. Zakaria aliipata barua,
akaisoma. Barua ilizungumzia mapenzi na Zakaria alikasirika zaidi. Alikwenda pamoja na Rosa nyumbani kwa mvulana aliyemwandikia Rosa barua. Mvulana huyo, aliitwa Charles. Zakaria alimtupia Charles shilingi, akamwambia kwamba hakutaka kumwona tena pamoja na binti yake.

Rosa Mistika alipata nafasi katika chuo cha ualimu baada ya matokeo ya darasa la 12.
 
R.I.P Profesa, kila mmoja wetu ataondoka wakati wake ukifika.
 
Back
Top Bottom