TANZIA: Mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa afariki dunia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Chama cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi kimepatwa na msiba kwa kumpoteza Mwenyekiti wa zamani na Muasisi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mzee Alhaj Ally Mtopa aliyefariki katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili leo asubuhi alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewapa pole wabunge kutoka mkoani Lindi kutokana na kifo hicho huku akisema kwamba Mzee Alhaj Ally Mtopa alikuwa miongoni mwa viongozi muhimu sana kwa nchi ya Tanzania.



FB_IMG_1523266357769.jpg
 
Poleni sana Wa a kilwa poleni sana wakazi wa Nanjilinji pole sana Sadati na Watoto wote wa mzeee mtopa
 
R.I.P Mzee mtopa utakumbukwa sana ,hasa siasa za 2015 ,kurudi nyuma ,wewe ndiye ulikuwa unamkingia sana kifua joka la mdimu (Membe) huko mikoa ya kusini na walikielewa sana

R.I.P Mzee
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom