TANZIA Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo auawa kikatili mjini Katoro

Status
Not open for further replies.

Kifai

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
816
172
Wakuu,

Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Busanda kupitia CHADEMA bwana Alphonce Mawazo afariki dunia leo.Chanzo cha kifo chake ni kutokana na kipigo kikali kutoka kwa kundi la vijana linalosemekana ni la green guard jana wakati akifanya kampeni kumnadi diwani wake.

Kamanda Mawazo pia ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita.

Kamanda Mawazo pia alikuwa ni member wa JamiiForums (Verified Member) kwa jina lake halisi la Alphonce Mawazo.


attachment.php

Marehemu Alfonce Mawazo, alizaliwa mwaka 1976 na kufariki mwaka 2015. Mwaka 2005 alijiunga na Chama Cha TLP ambapo hadi kufikia wakati huo alikuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Bondeni ya Jijini Arusha akifundisha masomo ya Hisabati na Kiingereza.

Kaatika mwaka huo, aligombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Sombetini (TLP) na kushinda nafasi hiyo ya udiwani na baadae mwaka 2007 alijiuzulu katika nafasi hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivyo kuifanya Kata hiyo kutokuwa na mwakilishi (Diwani) kwa muda wa miezi michache.

Hadi kufikia mwaka 2008, Halmashauri ya Arusha kwa kipindi hicho (sasa Jiji la Arusha), ilitangaza kufanya uchaguzi mdogo na kati ya watangaza nia alikuwemo marehemu, Alphones Mawazo, aliyegombea kwa tiketi ya CCM na alichaguliwa na wananchi kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine hadi 2010 ambapo ulifanyika uchaguzi Mkuu wakiwemo madiwani, Wabunge na nafasi ya Urais ambapo marehemu alishinda tena nafasi hiyo baada ya kugombea kwa tiketi ya CCM.

Taarifa za kuaminika zilizoifikia
FikraPevu zinaeleza kuwa mnamo mwaka 2011 akiwa mwanachama wa CCM na diwani wa kata hiyo, alijiuzulu nafasi yake na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lakini hakushiriki tena kutetea nafasi hiyo ya udiwani na badala yake aliongeza nguvu ya kutumikia chama hicho katika mikoa wa Kanda ya Ziwa.

Kata ya Sombetini ilikaa kwa zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchelewa kutangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kata hiyo hadi mwaka 2013 alipochaguliwa Ally Bananga kuwa diwani wa kata hiyo.

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kufanyika Bananga amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa mwakilishi wa wananchi kwa ngazi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Kisiasa marehemu Mawazo alikuwa swahiba mkubwa na mwanafunzi wa Godbless Lema tangu alipokuwa mwalimu. Lema ambaye kwa sasa anatetea tena nafasi ya kiti cha Ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini alikuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2010 na sasa anawania tena jimbo hilo.

Lema, walikuwa chama kimoja na marehemu Alphones. Mawazo aligombea udiwani kwa tiketi ya TLP mwaka 2005 (alichaguliwa kuwa diwani) huku Lema akigombea nafasi ya Ubunge kwa tiketi TLP Arusha mjini kwa kipindi cha mwaka huo huo (hakuchaguliwa).

Mwaka 2014, Alphonce Mawazo, achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita ambapo
inaelezwa kuwa alitumia muda mwingi sana na raslimali zake pale ilipohitajika kufanya hivyo Kuzunguka maeneo mbalimbali ya Taifa ili kuwapa Elimu ya Uraia hususani Watu wa Vijijini kwa kutumia usafiri mbalimbali ikiwemo Baiskeli.

Mwaka 2013, Mawazo alitoa gari lake akiwa Arusha na kuomba speaker na mafuta ya kumfikisha
Kanda ya Ziwa hasa vijijini ambako alisema ataenda kufia huko.

Mawazo alikuwa miongoni mwa vijana 7 Wa Chadema waliofanya vizuri 2013 nje ya Bunge. Mwaka 2011 kulitokea mapambano makali mkoani Arusha kati ya Polisi na wafuasi wa (CHADEMA) ambapo taarifa zilisema
Diwani wa Kata ya Sombetini (CCM) (kwa wakati huo), Alphonce Mawazo, alihamia CHADEMA akisema amechukizwa na ukatili wa CCM dhidi ya wananchi.

Alphonse Mawazo alikuwa mwanachama hai wa mtandao huu wa JamiiForums tangu mwaka 2013.

Soma
zaidi =>Mwenyekiti wa Chadema na Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Busanda auawa kikatili


Baadhi ya Mada alizowahi kuanzisha Marehemu Alphonse mawazo hapa JamiiForums ni:-

1. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...vyozuia-harakati-na-kuua-ndoto-za-vijana.html

2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-la-rorya-jioni-hii-kwa-operation-5-days.html

3. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...on-tigitigi-kwa-mikoa-mitano-yazinduliwa.html

4. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/693849-tatizo-la-ngombe-ni-kumpuuza-kupe-maishani.html


Mada juu ya Maoni ya Godbless Lema baada ya kifo cha Alphonce Mawazo - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wazo-ameuawa-na-mfumo-wa-jeshi-la-polisi.html

======

UPDATES

========

Washitakiwa wahukumiwa kifo. Zaidi soma:


Mawazoo.jpg
Mawazo.png
 
Mwenyekiti wa chadema mkoa wa geita na aliyekuwa anagombea ubunge kupitia chadema jimbo la busanda mkoani geita ajeruhiwa vibaya katika mji mdogo wa katoro na watu wanaosadikika ni vijana wa ccm

Hamjishughulishi na kueleza chanzo cha tukio, mazingira ya hilo tukio, mnachoona ni sahihi kwenu ni kusema "wanaosadikiwa kuwa vijana wa ccm"
 
Sad News: Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alfonse Mawazo amevamiwa na kuuawa...
mwenye habari zaidi atujuze mimi nime copy na ku paste tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom