TANZIA: Mwenyekiti wa baraza la wazee Kyela(CHADEMA), Anthony Mapunda afariki dunia

Friday Malafyale

JF-Expert Member
Jan 18, 2017
1,808
2,911
Mimi kama mzawa wa Wilaya ya Kyela na mwana CHADEMA nimesikitika kupata taarifa za kifo cha mzee Mapunda. Binafsi namfahamu vyema na mchango wake kwenye chama CHADEMA KYELA MBEYA.

Habari kamili iInaandikwa na Kwame Elly Anangisye Kada mwaminifu CDM
Mamia ya Wananchi wa Kyela - Mbeya tarehe 12 Machi, 2017 walikusanyika katika mazishi ya Antony R. Mapunda -Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Kyela na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Butiama kilichopo Kata ya Mbugani katika Mamlaka ya Mji wa Kyela.

Marehemu ambaye kipindi cha uhai wake alisifika kwa uongozi uliotukuka na msimamo wake thabiti kwenye mambo mbalimbali ya uongozi na utendaji, alikuwa ni mmoja wa waasisi wa Mageuzi nchini mwetu na kiongozi mahiri wa CHADEMA wilayani Kyela na pia wakati wa uhai wake Marehemu aliwahi kuwa Mchungaji wa Kanisa la T.A.G.

Msiba huo ambao ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kyela ambaye pia ni Mwanasiasa mkongwe Alipipi Kasyupa ambaye alitumia msiba huo kuiasa jamii kuiga mfano wa maisha ya Mzee Mapunda haswa kwenye suala zima la uchapakazi, msimamo na ujasiri wa kuitetea jamii katika kero mbalimbali.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa!


Matukio kwenye picha nime attach
0e20614f973105ad8fa335f2c5664e61.jpg


be3bc730fc130ae98ff845b5756be976.jpg


e6d95ba4f753608ecebe1d36b3471cf3.jpg


4e51a2bc7c39e33ea338f674bd35b32b.jpg


34b080efa7afad765e4d2189de17d3b0.jpg


0c74b8681545ad7eeb42db49f54e01cd.jpg


b67dc1e58297efec33c2ca0dd4a9f05f.jpg
 
Daaah kazikwa Mwamsungwi home kabisa!Kushoto kwa hayo makabuli kuna kabuli la Mzee wangu na ndipo home kwetu!
RIP Mapunda alikuwa rafiki yangu sana!Friday ulifika pale home kwa Shehe Mwaiposa japo kutembelea kabuli la mshua?
 
Mazishi ni mazishi tu! Hata kama yangezikwa kitajiri bado ni mazishi ni sawa na kufa.Kuna wakati jaribu kutenganisha mahusiano yako na itikadi ya chama chako na masuala ya kijamii.
Hamna ukweli tu usemwe,chama kile kina ukanda sana,sasa kikitokea arusha au kilimanjaro fuatilia itakuwaje wanahudumia vizur nje ya hapo kiaina.
 
Back
Top Bottom