TANZIA Mwanafunzi wa UDSM (COET) agongwa na gari

vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
6,311
10,349
Baada ya kupata huu ujumbe

Ndugu zangu wana UDSM nasikitika kuwapa taarifa kuwa jana usiku wa saa tano na dakika 20 nilishuhudia mwana UDSM mwenzangu akigongwa na gari ndogo nyeusi, maeneo ya njiapanda ya chuo Ubungo.

Gari iliyomburuza mita kadhaa kisha kusimama kurudi nyuma na kutokomea kusipojulikana baada ya makelele tuliyopiga. Mbaya zaida, gari la pili lililokuwa kasi nalo likamkanyaga kisha la tatu nalo likamkanyaga. Ndipo tulipoamua kusimama katikati ya barabara ili kuzuia maumivu zaidi kwa mtu ambaye mpaka wakati huo sikujua ni nani.

Nilikuwa mimi na naibu wangu, Joel Ntile, tukaamua kukata majani ili kuzuia magari yaliyokuwa yanakuja kwa kasi kutokana na kutokuwepo kwa foleni usiku ule katika barabara ya kutoka Mwenge kwenda Ubungo mataa.

Tukishirikiana na wananchi wengine, tulianza kutafuta gari la kumbeba huyu Mtanzania mwenzetu ambaye mpaka muda huo hatukujua ni nani. Lakini kila tuliyekuwa tukimwomba msaada hakutusaidia na nilipojaribu kupiga simu polisi, haikupokelewa mpaka tukapata akili ya kumkagua aliyegongwa kujua ana ndugu na jinsi gani watafika tushirikiane kumpa msaada. Mpaka muda huo, bado sikujua kuwa ninayemsaidia ni mwanafunzi mwenzangu.

Tulipoipata simu yake, tayari ilikuwa imezimika baada ya kupondwa na magari matatu, tukatoa line na kuiweka kwenye sim nyingine. Kila namba tuliyojaribu haikupokelewa. Wakati huo tuliadhimia kufunga barabara ili polisi wasikie japo kilio chetu, na kila tukipiga simu yao iliendelea kupiga wimbo uleule.

Mpaka tulifanikiwa kupata namba iliyoseviwa shem, tulipopiga alipokea na nilistushwa na kauli kuwa yupo mabibo na mwenye simu ni mwanafunzi mwenzake wa UDSM mwaka wa nne COET, nilivurugika akili.

Mpaka muda huo ilikuwa tayari saa nzima imepita bila msaada. Ndipo nikapiga simu haraka kwa rais wa DARUSO mh Ahadi Kitaponda, naye akatuma gari la wasaidizi wa polisi na dakika chache akaja na ambulance lakini mpaka muda huo tayari tulikuwa tumechelewa sana na mwanazuoni huyu alikuwa ameshaachana na ulimwengu huu wa shida na mateso.

Polisi walikuja baadae sana kama saa saba kasoro, wakiwa na bunduki na mabomu mithili wanakwenda kupambana na wahalifu, lakini kuja kwao hakukusaidia kitu. Ndipo tulianza kuandaa utaratibu wa kwenda kumpumzisha kwa muda ndugu yetu Muhimbili kwa kuanza na dispensary ya chuo na baadae mida ya saa tisa na nusu tukaingia Muhimbili tukiwa na viongozi wa DARUSO pamoja na jamaa na watu wa karibu wa marehemu na mpaka saa kumi na dakika arobaini tulikuwa tunarudi chuo na hatimaye Mabibo.

BWANA AMETOA NA BWENA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

NAWAOMBA WANAZUONI WENZANGU kupitia hili tujifunze kuwa kutembea na ID ni swala la muhimu na ukiweza bora uvae shingoni maana ndiyo inauwezo wa kuzungumza wewe usipokuwa na uwezo huo tena.

Pili, tunapoona mwanadamu yeyote kapatwa na madhila, tumsaidie bila kujali tunamfahamu au lah.

Mtoto wa dereva

Naamini mliomtendea hivyo damu yake haitowaacha daima.

Capture.PNG

Marehemu Egifrid August (24yrs) enzi za uhai wake.
 
Poleni sana Mulioguswa na kifi hiki. Tukio km hilu liliwahi tokea China. Ubinadamu unapotea. Angesimama dereva wa kwanza huyu kijanaangweza pona. Maeneo yenye mukusanyiko km Mlimani yahiraj CCTV cameras
 
r.i.p kijana wetu

mtoa mada umefanya jambo jema kutoa funzo ya kwamba tuwe tunatembea na vitambulisho popote,nami naongezea funzo lingine,wakati wa kuvuka barabara kunapokuwa na magari machache ni hatari zaidi maana magari huenda kasi zaidi na inapokuwa ni usiku hali huwa mbaya zaidi,tuongeze tahadhari zaidi ktk mazingira hayo tajwa

lakini mwisho wa maelezo yako binafsi sijayapenda

kwanini umetengeneza "roho" ya kisasi???kusoma kwako hadi chuo kikuu kunakufanya uamini dereva anaweza kufanya makusudi kumgonga mtu???na hata wa gari la pili na la tatu unaona nao wamefanya makusudi kumgonga?
 
r.i.p kijana wetu

mtoa mada umefanya jambo jema kutoa funzo ya kwamba tuwe tunatembea na vitambulisho popote,nami naongezea funzo lingine,wakati wa kuvuka barabara kunapokuwa na magari machache ni hatari zaidi maana magari huenda kasi zaidi na inapokuwa ni usiku hali huwa mbaya zaidi,tuongeze tahadhari zaidi ktk mazingira hayo tajwa

lakini mwisho wa maelezo yako binafsi sijayapenda

kwanini umetengeneza "roho" ya kisasi???kusoma kwako hadi chuo kikuu kunakufanya uamini dereva anaweza kufanya makusudi kumgonga mtu???na hata wa gari la pili na la tatu unaona nao wamefanya makusudi kumgonga?

Roho ya kisasi kwa vile amegonga halafu akatimua bila kusimama utadhani kagonga upepo au panya.!
 
Back
Top Bottom