TANZIA Mwanachama wa JamiiForums (kutoka JF Arusha Wing), Easymutant afariki dunia

Pumzika kwa Amani rafiki yetu kipenzi 😭😭😭😭😭
 
WanaJF,
View attachment 1235230
Taarifa nilizozipata ni kwamba, mwenzetu, Easymutant amefariki dunia usiku wa kuamkia Jana kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Sabble Square karibu na uwanja wa ndege wa Kisongo. Msiba upo Olasiti Arusha na updates zaidi nitawaletea hapa.

Poleni sana JF Arusha Wing na Members wote wa JamiiForums kwa ujumla.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

View attachment 1235020

Updates:

Mazishi ni kesho, mwili utachukuliwa Mount Meru Hospitali asubuhi saa 4 na kupelekwa nyumbani kwake saa saba mchana na kupelekwa kanisani Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Olasiti.

Maziko yatafanyika kwenye nyumba yake Mateves chini ya kituo cha mafuta cha OilCom Kisongo baada ya ibada.

Michango ya rambirambi inapokelewa na Hortensia Tarimo kwa namba 0759422471. Yeyote atakayeguswa anaweza kutuma rambirambi yake kwa namba hiyo!
RIP
 
Pole kwa wanafamilia ndugu,jamaa na marafiki. We loved you ila Yeye aliye na mamlaka kakupenda zaidi.Pumzika kwa amani mwanafamilia wa JF.
 
Nimelazimika kurudi hapa kwa haraka sana ili kuungana na wenzangu nyote kumlilia mwanaJF mwenzetu Easymutant.

Kifo chake kimekuwa si cha kawaida, maana kimetustua sana. Kwa ufupi hakuna aliyetarajia kuwa jamaa angeondoka katika siku za karibuni.

Arusha Wing tumepata pigo kuu maana huyu jamaa alikuwa ni mchezaji makini sana na alisaidia kutufanya Arusha Wing tuwe vile tunavyojulikana.

Kwasasa tunachofanya ni kumuombea kwa Mungu ili apokelewe salama.
Buriani Easymutant.
 
Mungu awape faraja wote walioguswa Kwa ukaribu kabisa na msiba wa member mwenzetu.
 
Nimelazimika kurudi hapa kwa haraka sana ili kuungana na wenzangu nyote kumlilia mwanaJF mwenzetu Easymutant.

Kifo chake kimekuwa si cha kawaida, maana kimetustua sana. Kwa ufupi hakuna aliyetarajia kuwa jamaa angeondoka katika siku za karibuni.

Arusha Wing tumepata pigo kuu maana huyu jamaa alikuwa ni mchezaji makini sana na alisaidia kutufanya Arusha Wing tuwe vile tunavyojulikana.

Kwasasa tunachofanya ni kumuombea kwa Mungu ili apokelewe salama.
Buriani Easymutant.
Pole sana rafiki,Umenitupa sana.
 
Namllilia ndugu yetu huyu, sikujua id yake humu before,nakiri kuwa alikuwa mwema kwa binadam wenzake, apumzike kwa amani rafiki mwema.
 
Back
Top Bottom