TANZIA Mwanachama na mfanyakazi wa JamiiForums, Dotto Mnzava afariki dunia kwa ajali ya pikipiki

Status
Not open for further replies.

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
attachment.php




attachment.php




Jamii Media Limited inasikitika kutangaza kuondokewa na mmoja wa wafanyakazi wake, Mwandishi Mkuu wa FikraPevu.com, Dotto J. Mnzava aliyefariki leo, Disemba 14, 2015 kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki na gari iliyotokea maeneo ya Victoria, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.


Mnzava alikuwa mwandishi wa Habari akiiandikia mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com na alijiunga na Jamii Media mapema mwaka jana, 2014.


Mipango ya mazishi na kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea kwao Same kwa ajili ya maziko inaendelea kufanyika na kwa sasa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Kuaga mwili kwa wakazi wa Dar kutafanyika Disemba 16, 2015 katika Kanisa la Waadventista Wasabato, Manzese (ulipo uwanja wa Tippi).


Tunatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto J. Mnzava.

Mungu amjalie pumziko la amani!


Amina

===================

Habari toka vyanzo vingine zaidi:


HABARI

Nimepokea taarifa za kushtua na zenye simanzi ambayo ni ngumu kufutika kichwani, tumempoteza kipenzi chetu, mwenzetu na rafiki yetu Dotto Mnzava. Dotto ni mwandishi wa habari na alikuwa anaenda kwenye mishe zake za kikazi, kutokana na foleni za Dar ikabidi achukue bodaboda (usafiri wa pikipiki).

Akiwa eneo la Victoria, pikipiki aliokuwa akisafiria ilipata ajali na yeye alianguka barabarani ndipo gari ikampitia kichwani na kusababisha mauti yake. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala kusubiri taratibu za mazishi.

BWANA AMETOA NAYE AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
BLOGGER chipukizi nchini Dotto Mzava, amefariki Dunia katika ajali ya barabarani Desemba 14, 2015 hapa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Nchini, (TBN), ambao marehemu alikuwa ni mwanachama wake, Bw. Joackim Mushi amesema Dotto ambaye alikuwa akifanyia kazi Jamii Media (Wamiliki wa mtandao wa
JamiiForums na Fikra Pevu, amefariki kwa ajali ya pikipiki ingawa haikuelezwa ajali hiyo imetokea maeneo gani hasa ya jiji la Dar es Salaam.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe Amin.

SOURCE: MICHUZI MEDIA


===================

UPDATE:
Habari za jioni WanaJamiiForums,

Mwili wa ndugu yetu Dotto Mnzava tayari umeagwa rasmi kwa hapa Dar-es-Salaam katika Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese karibia na uwanja wa TIPPI.

Mwili wake uko njiani unasafirishwa kuelekea nyumbani kwao Same Kilimanjaro kwa ajili ya kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Tunaendelea kuwakaribisha rafiki na ndugu wote wa Dotto Mnzava tuungane tukielekea kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.

Kwa maelezo zaidi piga namba: 0767 137 137
=====================

IMG_9145.JPG

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Dotto Mzava likishushwa Kwenye gari maalum mara baada ya kuwasili katika kanisa la Wasabato Manzese uzuri kwaajili ya sala ya kuombea kabla ya Mwili kusafirishwa kuelekea Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.


IMG_9166.JPG

Mchungaji wa kanisa la Adventist wasabato akiendelea na ibada wakati wa ibada ya kumuombea marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro


IMG_9175.JPG

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media Maxence Mello akitoa historia fupi ya Marehemu Dotto Mzava ambae pia alikua mmoja wa watumishi katika kampuni hiyo.


IMG_9181.JPG

Baba Mkubwa wa marehemu Dotto Mzava akitoa maneno ya shukrani katika kanisa la Kisabato la Manzese Uzuri mara baada ya zoezi la misa kumalizika.


IMG_9201.JPG

Heshima za Mwisho zikiendelea kutolewa


IMG_9187.JPG

Majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu


IMG_9204.JPG

Mmiliki wa Fullshangwe Blog, John Bukuku akitoa heshima za mwisho


IMG_9209.JPG

Heshima za mwisho zikiendelea kutolewa kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla haujasafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwaajili ya mazishi


IMG_9212.JPG

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla ya Kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarjiwa kufanyika kesho


IMG_9216.JPG

Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media akitoa heshima za mwisho kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa Same Mkoani Kilimanjaro mapema leo.


DSC_0334.JPG

Ibada ikiendelea


IMG_9235.JPG

IMG_9244.JPG

IMG_9254.JPG

Jeneza lenye mwili wa marehemu Dotto Mzava likipandishwa ndani ya gari tayari kwa safari ya kuelekea Same Mkoa wa Kilimanjaro leo kwaajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho


 

Attachments

  • Dotto_Mnzava_Pavillion.jpg
    Dotto_Mnzava_Pavillion.jpg
    31.5 KB · Views: 10,601
  • index.jpeg
    index.jpeg
    27.5 KB · Views: 4,805
HABARI
attachment.php

Nimepokea taarifa za kushtua na zenye simanzi ambayo ni ngumu kufutika kichwani, tumempoteza kipenzi chetu, mwenzetu na rafiki yetu Dotto Mnzava. Dotto ni mwandishi wa habari na alikua anaenda kwenye mishe zake za kikazi. Kutokana na foleni za Dar ikabidi achukue boda boda. Akiwa eneo la Victora, pikipiki aliokuwa akisafiria ilipata ajali na yeye alianguka barabarani ndipo gari ikampitia kichwani na kusababisha mauti yake.

BWANA AMETOA NAYE AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
 

Attachments

  • profilepic213201_2.gif.png
    profilepic213201_2.gif.png
    85.6 KB · Views: 11,495
Wakuu kuna taarifa zimeenea kuwa member mwenzetu Dotto Mnzava kafariki kwa ajili.

Mwenye taarifa rasmi tunaomba kujulishwa.
 
Last edited by a moderator:
HABARI

NIMEPOKEA TAARIFA ZA KUSHTUA NA ZENYE SIMANZI AMBAYO KUFUTIKA KWAKE KICHWANI HAKUTAISHA KAMWE
TUMEMPOTEZA KIPENZI CHETU MWENZETU RAFIKI YETU Dotto Mnzava INAUMA SANA YANI HATA MPAKA SASA
SIAMINI KWELI DOTTO AMETUTOKA HIVI; NASHINDWA HATA KUANDIKA HAPA
AMEFARIKI MAENEO YA VICTORIA KWA AJALI YA PIKIPIKI, TAARIFA KAMILI TUTAZIPATA KUTOKA KWA NDUGU ZAKE NA WALE WALIOKARI NAYE


MUNGU AWAPE FARAJA NA KUWAPA NGUVU FAMIILIA ALIYOIACHA, NDUGU PAMOJA NA
UONGOZI WOTE WA JAMIIFORUM

BWANA AMETOA NAYE AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE




attachment.php
 
Wapendwa wana Jf, ni masikitiko makubwa kuwajulisha kifo cha member mwenzetu hapa Jf Dotto Mnzava kilichotokea leo mchana saa 8 baada ya kupata ajari ya Pikipiki maeneo ya Victoria jijini Dar.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa ktk hospital ya mwananyamala kusubiri taratibu zitakazofata.

Pumzika kwa amani rafiki yangu Dotto.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom