TANZIA: Mwanachama mwenzetu, PakaJimmy amefiwa na mwanae ajali ya basi Arusha

Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
24,685
28,769
Arusha wing tunasikitika kutangaza kifo cha mtoto wa member mwenzetu PakaJimmy kilichotokea leo hii kwa ajali ya basi la shule,ni kati ya wale wanafunzi wa Lucky Vincent...

Ni msiba mzito mno mno kwa mzazi yeyote kumpoteza mtoto hasa katika mazingira kama haya ya ghafla,unaagana na mwanao vizuri asubuhi ghafla unasikia amezimika kama mshumaa. Msiba upo nyumbani kwake kwa mromboo, PJ rafiki zako tuko nawe katika hili,

Ni majonzi makubwa mno... Arusha wing tunaungana na wote waliokumbwa na msiba huu mkubwa,Mwenyezi Mungu awatie nguvu,tuko pamoja kwenye hili...

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe...

Baada ya baadhi kuomba no ya mchango tunaomba michango yote ielekezwe kwa 0754288808 jina la usajili ni Pamela Lyamuya... No hii ndo imeteuliwa na Arusha wing kupokea michango

--
Katika hatua nyingine, Roland Mwaliambi anayeishi Dar es Salaam alisema kwa mara ya kwanza alipata taarifa ya ajali hiyo kupitia WhatsaApp kabla ya watoto wake waliopo jijini hapa kumpigia simu.

Alisema baada ya taarifa hiyo alilazimika kuchukua usafiri wa haraka wa ndege kuwahi Arusha ambako alithibitisha kwamba mwanae Praise ni miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo.

Alisema mwanae ambaye alionyesha kuwa na wito wa upadre alitarajia kujiunga na Seminari ya Maua iliyopo Moshi Januari mwakani na taratibu zilikwishafanyika za kujaza fomu ya maendeleo yake kitaaluma, lakini ndoto yake imezimwa ghafla.

Chanzo: Nipashe

Cc Preta Filipo marejesho LiverpoolFC n.k
 
Back
Top Bottom