TANZIA: Mwana JF mwenzetu Jeska amefiwa na mama yake mzazi huko Bukoba

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000
Ni matumaini yangu kwamba wote ni wazima wa afya.

Nimepata taarifa asubuhi ya leo kwamba mwana JF mwenzetu Jeska amefiwa na mama yake mzazi huko Bukoba hapo mnamo tarehe 21 May 2014 na amekwishaondoka kwenda Bukoba kuhudhuria mazishi ya mama yake.

Ukweli ni kwmaba nilichelewa kupata hizo taarifa kwa sababu na miye nilikuwa nje ya mkoa na huko nilikokuwa network ilikuwa inasumbua na ndiyo sababu nikachelewa kupata taarifa. Naamini mama yetu atakuwa ameshapumzishwa kaburini na siye kama familia tumuweke mwana JF mwenzetu Jeska katika maombi.

Kwa sasa najaribu kumtafuta mtandaoni simpati nadhani inaweza kuwa ni network maana sijajua ni Bukoba sehemu gani, lakini nitakapopata taarifa zaidi nitawajulisha.

Raha ya Millele Umpe Ee Bwana Na Mwanga wa Milele umuangazie, Apumzike kwa Amani.

Amina.

CC:
Kaizer, Paloma, Ennie, Lisa, Ruttashobolwa, Asprin, KakaKiiza, Maxence Melo, gfsonwin, cacico, Bujibuji, Kiranga, Nyani Ngabu, The Boss, BADILI TABIA, snowhite, Fixed Point, Nivea, Tina, lara 1, King'asti, Mwita Maranya, charminglady, Asnam, Elizabeth Dominic, Arushaone, Nicas Mtei, Munkari, MankaM, Heaven on Earth, Asprin, Filipo, Preta, Mungi, Don Mangi, Lady doctor, mayenga, mwekundu, figganigga. Samahani nimewataja wachache lakini naamini wote kwa pamoja ujumbe huu utawafikia
 

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,089
2,000
Ahsante kwa taarifa Mkuu,bila shaka utajitahidi kutupatia taarifa zaidi ili tupange pamoja tukamfariji.Ahsante
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,727
2,000
Mungu akupe moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu sana kwako Jeska

Nasi tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu amrehemu mama yetu Mpendwa.

Alale pema peponi mama yetu.
 
Last edited by a moderator:

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,361
2,000
Anapitawakatimgumu sana sijapata kuomba unirudie tena


Mungu akuhifadhi nakukulinda mumlaze salama nyumba yake ya milele
Bwana ametoa Bwana Ametwaaa Ninakelihimidiwe
 

Paloma

JF-Expert Member
Jan 22, 2008
5,335
1,195
ooh maskini! Pole sana Jeska, mwenyezi mungu wapeni faraja.
Mama Jesk pumzkawka amani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom