TANZIA: Mwana JamiiForums mwenzetu Musa Maya amefiwa na mdogo wake

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,895
25,944
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu

Kwa maskitiko makubwa na majonzi makubwa sana jaman mwana jamiforums mwenzetu mussa maya kafiwa na mdogo wake kipenzi huko Dar na mazish yatakuwa leo temeke

Kwa wale ambao tuko Dar tumpe ushirikiano mshikaji wetu

Pole sana ndugu yangu Mussa Maya, poleni sana na familia kwa ujumla

Bwana alitoa na bwana ametwaa.

pole sana Mussa
 
Mungu awafanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu.
 
Hili suala la kuzika binadamu mapema huwa linanipa ukakasi sana. Kuna uwezekano huwa tunazika watu wakiwa wazima. Case and point, yule mwanafunzi ambaye alifananishwa na Panya road kule mbagala. Alipokea kipigo mpaka akapoteza fahamu na kupelekea watu kudhani ya kwamba amefariki. Alipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Temeke. Baada ya muda alizinduka na kuzua taharuki kubwa sana.
 
Sasa kama mgonjwa kafia hospital na daktari kathibitisha kwanini wasizike mapema

R.I.P
 
Sasa kama mgonjwa kafia hospital na daktari kathibitisha kwanini wasizike mapema

R.I.P
Ni nani aliyekuambia amefia hospitali? Kwani yule mwanafunzi aliyezinduka katika chumba cha maiti katika hospitali ya Temeke Madaktari hawakuthibitisha kwamba amefariki? Madaktari ni binadamu na kuna kitu kinaitwa "human error". Wana changamoto nyingi sana, ikiwamo kuhudumia wagonjwa wengi na masaa mengi kazini. Tumia akili ya ziada kuchanganua mambo ya msingi ndugu, achana na tabia ya kukurupuka ili uonekane nzawisa.
 
Back
Top Bottom