TANZIA: Muasisi wa CHADEMA, Mzee Victor Kimesera afariki dunia

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
KISESERA.JPG

Mzee Kimesera enzi za uhai wake
Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa siasa za vyama vingi hapa Tanzania na mwanachama/kiongozi mwandamizi wa CHADEMA, amefariki dunia usiku huu jijini Dar Es Salaam.

Kimesera aliwahi kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiteto,uchaguzi ambao ulikuwa na ushindani mkubwa sana na hatimaye CCM kuibuka na ushindi.

Ni mmoja kati ya Wazee wenye misimamo na wasioyumba,hata katika magumu ya siasa za upinzani hapa Tanzania,Kimesera aliendelea kuwa ndani ya CHADEMA,wakati wa uchaguzi mdogo wa Kiteto,Mzee Kimesera aliugua dakika za mwisho na kugundulika amepewa sumu na hivyo kuzua taharuki kubwa sana.

Upumzike kwa amani Mzee Kimesera

Pia soma...
- Mzee Victor Kimesera: Mzee Ndesamburo aliiwezesha CHADEMA kununua ofisi ya makao makuu
- KLH Exclusive: Victor Kimesera live
 
Mmoja wa Waasisi wa CHADEMA , Mzee Victor Kimesela amefariki dunia jioni hii katika Hospitali ya Muhimbili.
Msiba upo nyumbani kwake Victoria mtaa wa uporoto nyumba no 52.
 
..Mzee Victor Kimesera.

..CDM imepata pigo kubwa sana.

..MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.
 
Umepigana vita vilivyo vema!..Pumzika kwa amani!!..
 
R.I.p mzee tutakukumbuka sana hasa kwa misimamo yako isiyoyumba maana slow slow alikutangazia dau nono lakin ulilikataa

mbele yako nyuma yetu ulale mahala salama pepon
 
Mmoja wa Waasisi wa CHADEMA , Mzee Victor Kimesela amefariki dunia jioni hii katika Hospitali ya Muhimbili.
Msiba upo nyumbani kwake Victoria mtaa wa uporoto nyumba no 52.


Ni siku ya huzuni kweli, alikuwa ni miongoni mwa vinara wa upinzani Tanzania na mchango wake kwa kweli ni wa kukumbukwa na kuenziwa. Mungu ailaze roho yake pema peponi, na awape faraja wafiwa wote. Amina.
 
R.I.P MZEE KIMESERA...

Mzee_Victor_Kimesera, mmoja wa waasisi wa siasa za vyama vingi hapa Tanzania na mwanachama/kiongozi mwandamizi wa CHADEMA, amefariki dunia usiku huu jijini Dar Es Salaam.

Jamani hapa duniani hakuna atakayedumu, Mzee Victor nashindwa hata kuelezea...ni mmoja wa wazee ambao asingelishindwa kukupa msaada wa fikra kwa jambo lolote lile linalokusumbua.

Alikuwa mwerevu wa maarifa na asiye na mkono wa birika kusambaza maarifa hayo kwa kila muhitaji. Mwaka huu nchi yetu imepoteza watu muhimu sana.

R.I.P Mzee Kimesera,
Poleni sana wanafamilia,
Pole sana Comrade Freeman na wana Chadema wote.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
[HASHTAG]#Mwenyekiti[/HASHTAG] wa Kamati ya Uongozi,
[HASHTAG]#The[/HASHTAG] Civic United Front.
#24 Machi 2018.
 
Dah hata nimeishiwa maneno kwa kweli RIP Mzee wetu nakumbuka sana ulivyosimama na chama hasa kipindi cha migogoro ile ya kuelekea uchaguzi wa ndani 2014..... RIP wana mabadiliko wote tutakukumbuka daima
 
Back
Top Bottom