TANZIA: Mtangazaji wa Kituo cha Runinga cha Star Tv, Radio Free Africa Samadu Hassan afariki dunia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mtangazaji maarufu na Mkongwe wa Habari za Kimataifa wa kituo cha Runinga ya Star Tv na Radio Free Africa, (Sahara Media Group) Samadu Hassan amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo.

Alikuwa akitangaza kituo cha Radio Abood FM kilichopo mkoani Morogoro baada ya kutoka Star Tv na Radio Free Africa.

Samadu aliyewahi kufanya kazi nchini Kenya alijiozolea umaarufu kutoka na sauti yake ya kipekee na umahiri wake katika kutangaza habari, hasa duru za kimataifa.

Inadaiwa amefariki ghafla nyumbani kwake eneo la Miembe Mitatu, Nyamagana jijini Mwanza, baada ya kubanwa na maumivu ya kifua.
IMG_20181101_065438.jpeg

Mtangazaji maarufu wa kituo cha Star TV na Radio Free Africa, Samadu Hassan amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake eneo la Miembe Mitatu, jirani na kituo cha Chakechake wilayani Nyamagana jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi Digital asubuhi hii, mdogo wa Samadu, Latifa Hassan amesema kaka yake alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa zaidi ya wiki moja, kabla ya kufikwa na umauti usiku.

“Samadu alirudi nyumbani kwake jana jioni, akitokea kazini na alikuwa mzima wa afya, japo alikuwa akilalamika kuwa kifua kilikuwa kinamsumbua kwa takriban wiki nzima sasa,” amesema Latifa.

“Tulikuwa na maongezi naye kwa muda na baadaye tukala naye chakula hadi tukamaliza, akatueleza kifua kinamsumbua, tukamshauri pengine twende hospitali usiku huo kupata matibabu akasema angeenda kesho (leo).”

Hata hivyo anasema ilipofika saa sita kasoro usiku, ghafla hali yake ilianza kubadilika na alianguka chini na kuanza kutokwa na mapovu mdomoni.

“Hali hiyo ilitufanya tukimbie kwenda kutafuta gari ili kumuwahisha hospitali, lakini hadi tumepata gari na kurudi ndani tukakuta tayari ameshafariki,” amesema Latifa.
 
Mtangazaji maarufu wa habari za kimataifa kutoka kampuni ya Sahara ndugu Samadu Hassan ametangulia mbele za haki
IMG_20181101_051554_355.JPG
 
Back
Top Bottom