Tanzia: Mtangazaji wa DW, Mohammed Dahman afariki dunia

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,680
22,685
Taarifa za kifo cha mtangazaji mwenzetu Mohammed Dahman, aliyeaga dunia siku ya Ijumaa (02.08.2019) mjini Cologne, magharibi mwa Ujerumani, zimeishtua timu nzima ya Idhaa ya Kiswahili ya DW mjini Bonn.
Screenshot_20190803-161638~2.png

Mohammed alikuwa mwandishi habari mahiri katika nyanja zote, lakini alipendelea sana taarifa ya habari za ulimwengu na makala ya mbiu ya mnyonge.

Asilimia kubwa ya wasikilizaji walizipenda sana makala zake kuhusu masuala ya haki za binadamu na sauti yake ya huruma. Aliwapa sauti wasiokuwa na saut, hakukata tamaa kuwatafuta watu muafaka wa kuwahoji na alikuwa makini sana katika kuhakikisha taarifa zake pamoja na makala haziegemei upande mmoja.

Kama mwandishi, Mohammed alikuwa mfano wa kuigwa kwa wengi wetu. Amekuwa akiugua kwa kipindi cha takriban miaka miwili na muda wote huu hakuweza kufanya kazi. Hata hivyo hatukukata tamaa kwamba angepata afueni na kurejea kazini kujumuika nasi kuendelea na majukumu yake.

Katika wakati huu mgumu wa majaribu, fikra na dua zetu tunazielekeza kwa mke wake, binti yake na familia yake visiwani Zanzibar na ughaibuni. Tunawapa pole na kutoa rambirambi zetu kwa majonzi makubwa, machozi yakitiririka machoni mwetu. Tunawaombea. Tulimpenda, lakini Mungu amempenda zaidi.

Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt, na wafanyakazi wote wa idhaa hii mjini Bonn tunawapa pole jamaa, marafiki na mashabiki kwa kuondokewa na mpendwa wetu.

(Andrea Schmit; Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW)
 
Rest in peace Mohamed

Nilikuwa nasikiliza Dw saa saba mchana primary ilikuwa muda wa mapumziko ya chakula cha mchana. Basi kule kijijini tulikuwa tunarud home kula kisha kurud tena shule. Tukifika tuu redio station ni dw. Ilinifanya nijue somo la maarifa ya jamii.
 
Kama ni yeye kweli ninavyomjua sidhani kama hiyo picha ndo yeye labda huyo ni mwingine majina kufanana
 
Kwani yule mohamed ambae kwa sasa ameshastaafu alikuwa na sauti nzito nzito fulani nae ni mwingine tofauti na huyu au ni wawili tofauti
 
Back
Top Bottom