Tanzia: Msanii Mashaka (Ramadhani Ditopile) wa Kaole Sanaa Group afariki dunia

Eli wallach

Member
Oct 17, 2018
25
21
TAARIFA:

Mashaka aliugua ghafla usiku ndipo wakamkimbiza hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu na ilipofika asubuhi hali yake ikabadilika. Madaktari walitoa rufaa ya kumpelekea katika Hospitali ya Muhimbili (Tawi la Mloganzila), wakati ikitafutwa ambulance, akakata roho.

Mashaka alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Presha pamoja na kisukari ambapo jana alizidiwa gafla na kukimbizwa hospitali, madaktari walifanikiwa kumpa huduma ya kwanza na matibabu ikiwa pamoja na kumuwekea mashine ya kupumulia ya oksijeni.

FB_IMG_1540030427618.jpg
 
Kwa kweli ni huzuni moyoni kumpoteza baba yangu wa hiari mzee Mashaka, huyu mzee alikuwa na roho ya kipekee sana kila mtu alimpenda mazishi yatakuwepo ilala bungoni japokuwa kwake ni ubungo kibo..inauma sana mzee umefariki ghafla ingali bado wanao tulikuwa bado tunakutegemea
 
Back
Top Bottom