kunguni wa ulaya
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 4,132
- 6,100
Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, AliKiba (Mzee Saleh Kiba) amefariki Dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Taarifa kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa baada ya ndugu kukutana na kufanya mipango.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMIN
RATIBA YA MAZISHI YA BABA YAKE ALIKIBA
________________________________
Maiti itaswaliwa katika msikiti wa Madina - Tandamti Kariakoo - saa 10 jioni, kisha mazishi yatafanyika makaburi ya Kisutu baada ya sala!