Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 150
- 176
Habari za muda huu zinaeleza kuwa Mpoki Bukuku, mpigapicha mkuu wa magazeti ya IPP, amefariki dunia.
Jana usiku alipata ajali akiwa anarejea nyumbani kutokea kazini.
Alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa zaidi baadaye
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuondokewa nduguyetu, Mwanahabari Mpoki Bukuku. Katika kipindi ambacho tasnia ya habari inapitia kipindi chenye changamoto lukuki tulihitaji sana kuwa naye. Mwenyezi Mungu kamruhusu mwanaye, aende karibu na hukumu zake. Kila la kheri Kaka, mbele umetutangulia. Tunamrudishia Bwana sifa na utukufu. Sisi sote ni waja.
========
Mpigapicha maarufu, Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI) alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu. Mpoki alifikishwa MOI jana usiku baada ya kupata ajali ya gari eneo la Mwenge-ITV na kujeruhiwa sehemu mbalimbali.