TANZIA: Mpiga picha maarufu, Mpoki Bukuku amefariki dunia

KAPUMZIKE KWA AMANI, MWANGA WA MILELE UKUANGAZIE NA UPATE RAHA YA MILELE.

AMEN
 
Poleni wafiwa.Alikuwa role model kwa wengi katika kazi yake ya fotojounalism.Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina la Bwana lihimidiwe.
 
Mpigapicha maarufu Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.

"Ni kweli Mpoki amefariki dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo la Mwenge ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadaye," alisema Almas.

Mpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, linalochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Pia amewahi kufanya kazi magazeti kadhaa likiwemo Majira na Nipashe.

Chanzo:Mwananchi
 
Back
Top Bottom