G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Imeripotiwa muda mfupi uliopita kuwa Pendo Butenghe ambaye ni Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kagera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Akithibitisha kifo hicho, Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fush, amesema marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kushuka sukari mwilini.
Taarifa rasmi za kilichomuua hazijatolewa.
===
Mkuu wa Uhamiaji mkoani Kagera Pendo Butenghe, amefariki usiku wa kuamkia leo, Aprili 29 katika Kliniki ya COSAD kutokana na maradhi ya Shinikizo la Damu na Kisukari
Aidha, inadaiwa marehemu alianza kutumia dawa za kienyeji (kujifukuza) na alipoanza kukosa pumzi na kushindwa kuhema mkewe alimpeleka katika Kliniki hiyo. Aliwekewa drip lakini kupumua ikawa shida zaidi hadi akakutwa na mauti
Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fush, amesema wanasubiria mwongozo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Makao Makuu ya Uhamiaji kujua taratibu za msiba na maziko