TANZIA: Mhadhiri wa Chuo Kikuu na Mwandishi wa vitabu Dominic Thabit Msabila afariki dunia

Msabila alijitahidi sana kusummarize vitabu kama Bunnet na vingine vikubwa vya Geography ambavyo huenda vingekuwa complicated kwa wengi.
 
Ni huzuni na kilio kisicho na kifani kuondokewa na mwalimu, mwandishi mahiri wa somo la Geography (Physical na Human) ndugu yetu Dominic Thabit Msabila (D.T).


Mwalimu Msabila kwa kutumia kalamu yake amewasaidia vijana wengi kwa kutoa vitabu vyake kupitia kampuni ya Nyambari Nyangwine Publishers.

Mwalimu Msabila amekuwa Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe akifundisha kozi za lugha na lugha ya kisheria.

Bwana ametoa na bwana ametwaa, Amina

DT Msabila apumzike kwa amani
 
Ni yeye mkuu mimi nafanya kazi na Partener wake kwenye hiyo kazi ya uandishi jamaa ameomba ruhusa kazini kwenda kuzika swahiba wake by the way kama kunamtu kasoma geography Tanzania hii miaka ya 2000 siyo rahisi kwamba hujawahi kutumia kitabu cha mdabila. Advance physical geography ni moja ya kazi zake mahiri sana, atakumbukwa kwa vizazi kupitia kazi zake
Mbona kuna wanaokanusha na kusema si yeye ila ni ndugu yake
Screenshot_20191031-191700.jpeg
 
Dah R. I. P mwalimu. Tumetumia sana vitabu vyako. Dah utakumbukwa kwa hilo sanaa
 
Hivi necta na wizara ya elimu wameongea lolote juu ya huyu nguli wa geography?? R.I.P
 
Wakenya wanasema watanzania tunapenda udaku hatupendi vitu vinavyogusa maisha yetu,mwaka huu nakumba kuna member alileta taarifa ya kifo cha mwalimu wa somo la English pale Meta sec au Iyunga kwa namna alivyokuwa anachangiwa humu jukwaani alistahili apeweheshima zake kwa sababu wengi walipikwa kupitia yeye lakini maskini alizikwa kimyakimya tu hivyo watanzania tunapenda vitu vidogovidogo .
 
R.i.p.
Km hujapita skuli hata kidogo...huwezi elewa how Important he was
Your thoughts will remain forever
 
Rip mwalimu

Kusoma nimesoma lakin sijui hata kama nilikuwa natumia vitabu vyako

Shule za kata hizi jaman
 
Sawa mkuu lakini amini maswali yote ya fluid mechanics ya muncaster nliya solve

Yote mkuu.... Maswali ambayo nliicha baadhi ni electronics ya muncaster

Hasa kwenye operational amplifier kuna swali la kimbanda sana pale
Niliyagongaga maswali yote ya Gravitational ya Roger muncaster..daaah ila UNIVERSITY PHYSICS nilinyanyuaga mikono..mhhh
 
Allah amuweke panapostahiki. Kama ni kafiri ataenda motoni tuu hata kama kafanyeje.. Bac ni hayo tuu
 
Nimehuzunika sana. Hayati Msabila ndiye aliye edit thesis yangu. Bwana ametoa,Bwana ametwaa,jina la Bwana lihimidiwe. Mungu akawe mfariji kwa familia yake na wote walioguswa na msiba wa Hayati Msabila.
 
Simjui hanijui ila kwa kusema kweli vitabu vyake vimenitoa jalalani ,o'level nimesoma Sana'a vitabu vyake hadi basii
 
Hakika ulikuwa msaada kwetu kupitia vitabu vyako ulivyoandika kwa mpangilio mzuri na wenye mantiki.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Hakika umefanya kazi kubwa kwenye elimu yetu ya Tanzania.🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom