dingihimself
JF-Expert Member
- Jan 9, 2016
- 9,399
- 19,418
Mchungaji na mwalimu Dkt. Peter Mitimingi wa Kanisa la Ghala la Chakula au kwa kimombo “Warehouse Christian Centre(WCC)” amefariki dunia, usiku huu. Mchungaji Mitimingi alizaliwa mwaka 1975.
Kabla ya kuanzisha kanisa lake hilo, alihudumu TAG kama mchungaji msaidizi na baadaye kuanzisha huduma ya injili vijijini.
Mch. Mitimingi anadaiwa alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa, Muhimbili na Kafariki saa Tisa za alasiri
Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo Samwel, amethibitisha. “alikuwa anaumwa Sukari ilipanda, ikaanza homa ya mapafu kwasababu alikuwa Arusha akapigwa na mvua kukawa na baridi kali ikamsumbua”
Kaacha Mke na Watoto Wanne.
WASIFU WA MAREHEMU
KUZALIWA
Machi 03, 1975 -mkoani Tabora
ELIMU
Stashahada (Diploma) ya Elimu ya Kikristo - ICM Seminary Kenya.
Shahada (Bachelor) ya Biblia na Theolojia - Africa Theological Seminary - Kenya
Shahada uzamili (Masters) ya Ushauri na Saikolojia - Uganda Christian University
Shahada ya Uzamivu (PHD) - Africa Graduate Universty - Sierra Leone
KAZI
- Mchungaji
- Mkufunzi
- Mwandishi wa Vitabu (ameandika vitabu zaidi ya 40)
- Mshauri wa saikolojia na Biblia
- Mhadhiri wa Chuo Kikuu
KUFARIKI
May 3, 2020 - Hospitali ya Muhimbili Familia
FAMILIA
Ameacha Mke na watoto wa 4
--
VIDEO: Kauli yake kuhusiana na Ugonjwa wa Corona
Marehemu Mchungaji Mitomingi, wiki tano zilizopita alipakia picha mbalimbali kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa anafanya ziara nje ya nchi ambapo alikaa kwa siku kadhaa na kurudi nchini. Baada ya kurudi nchini pia alipakia picha akionesha kuwa ameamua kujitenga(Karantini) ili kuweza kujua mwenendo wa afya yake kuhusu maambukizi ya Virusi vya Corona. Baadaye aliendelea kutoa huduma ya kiroho kwa waumini wake mpaka hapo alianza kuumwa na umauti kumkuta akiwa anapatiwa matibabu ya homa ya mapafu.
Baadhi ya mada zilizoanzishwa JF kuhusu alichokuwa anakifanya
- Mchungaji Mitimingi yeye ni mchungaji wa mapenzi tu? Wito wake uko kwenye mapenzi?
- Mahubiri ya Mchungaji Peter Mitimingi ni hazina kwa vijana na watanzania kwa ujumla
- Mchungaji Mitimingi: Ogopa sana mwanamke mwenye tabia ya kuiga maisha ya marafiki zake
- Mchungaji Peter Mitimingi acha kupotosha wanawake
- Mchungaji Mitimingi: Kibamia siyo tatizo la mwanaume kushindwa kumlidhisha mwanamke kingono
Kuanzisha “Warehouse Christian Centre(WCC)”
Baada ya kutumika katika kanisa la Tanzania Asseblies of God (TAG ) zaidi ya miaka ishirini Mchungaji Mitimingi alizindua kanisa lake Jijini Dar es salaam ambapo alinukuliwa na vyombo vya habari kueleza kuwa hakuondoka kwa ugomvi.
"Sijatoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa ugomvi kama watu wanavyozusha bali nilikwenda kwa viongozi wa juu wa Kanisa. Nilianza na nyumbani Mwenge TAG ambapo nilikuwa mchungaji msaidizi, nikaenda kwa mchungaji wa wilaya, nikaenda kwa Makamu wa Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dkt. Magnus Mhiche. Wote hawa walinikubali, wakaniombea na kuniwekea mikono tayari kwa kutumika." Alisema Mitimingi.
UPDATE: 06 Mei, 2020 - MAZISHI