TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania Ally Yusuph Tigana, amefariki dunia

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
Mchezaji wa zamani aliyewahi kuzichezea timu za Simba na Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania Ally Yusuph Tigana, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.
PIC+TIGANA.jpg
Tigana-1.jpg
 
1575558702267.png

Kiungo wa zamani wa Yanga, Ally Yusuf ‘Tigana’ amefariki dunia leo Alhamis mchana katika hospitali ya Amana, Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa hospitali hapo.

Akithibisha kifo hicho, mchezaji Lubigisa Lubigisa alisema ni kweli Tigana amefariki leo mchana baada ya kuugua ghafla kuhara na kutapiki na kukimbizwa hospitali ya Amana ambako mauti yamemkuta.
1575558744560.png

Lubigisa alisema awali mke wa Tigana ndio alikuwa akiumwa na alikuwa amelazwa Amana, hivyo jana Jumatano alipokwenda kumuangalia hali ya mchezaji huyo ikaanza kubadilika.

"Alipofika nyumbani hali yake ikabadilika, akaanza kutapika na kuharisha kisha kukimbizwa hospitalini Amana, lakini baada ya kufika hapo alizidi kubadilika zaidi kutokana na kutapika akazidi kuishiwa nguvu," alisema Lubuigisa.

Aliongeza kutokana na hali alizidi kupungua hadi mauti yalipomkuta mchezaji huyo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom