TANZIA: Mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga pamoja na timu ya taifa ya Tanzania Ally Yusuph Tigana, amefariki dunia

Baharia Wa Buza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Messages
753
Points
1,000

Baharia Wa Buza

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2019
753 1,000
1575558702267.png

Kiungo wa zamani wa Yanga, Ally Yusuf ‘Tigana’ amefariki dunia leo Alhamis mchana katika hospitali ya Amana, Jijini Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa hospitali hapo.

Akithibisha kifo hicho, mchezaji Lubigisa Lubigisa alisema ni kweli Tigana amefariki leo mchana baada ya kuugua ghafla kuhara na kutapiki na kukimbizwa hospitali ya Amana ambako mauti yamemkuta.
1575558744560.png

Lubigisa alisema awali mke wa Tigana ndio alikuwa akiumwa na alikuwa amelazwa Amana, hivyo jana Jumatano alipokwenda kumuangalia hali ya mchezaji huyo ikaanza kubadilika.

"Alipofika nyumbani hali yake ikabadilika, akaanza kutapika na kuharisha kisha kukimbizwa hospitalini Amana, lakini baada ya kufika hapo alizidi kubadilika zaidi kutokana na kutapika akazidi kuishiwa nguvu," alisema Lubuigisa.

Aliongeza kutokana na hali alizidi kupungua hadi mauti yalipomkuta mchezaji huyo.
 

Forum statistics

Threads 1,379,670
Members 525,486
Posts 33,752,986
Top