TANZIA: Mbunge wa Geita Mjini, Donald Max afariki Dunia

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,204
7,892
Habari mbaya, mbunge wa jimbo la geita bwana Donald Max amefariki dunia hivi punde. Pole kwa wananchi wa Geita
donald.jpg


Siku za nyuma ilishawahi kuletwa thread JamiiForums akiwa India alipokua anatibiwa kansa ya Ubongo.
https://www.jamiiforums.com/habari-...bunge-donald-max-aingizwa-icu-hali-mbaya.html

Max.jpg


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita (CCM) Mheshimiwa Donald Kevin Max (58)(picha) amefariki dunia.

Kufuatia taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) kwa Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na umma kwa ujumla, Mhe. Max amefariki dunia tarehe 23 Juni, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia kadri zitakavyopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba ya Mazishi.

"BWANA ametoa, BWANA ametwaa,
Jina la BWANA lihimidiwe." Amina.

Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,

DODOMA

=====================

Updates

Spika wa Bunge Anna Makinda, ametangaza leo tarehe 24 asubuhi Bungeni kwamba, amefariki jana saa za mchana baada ya kuwa amelazwa kwa muda mrefu. Taarifa za awali ni kwamba Marehemu atazikwa Dar Es Salaam siku ya Jumamosi. Spika kasema taarifa nyingine bado anaendelea kuwasiliana na familia.

Spika kasema kwa mujibu wa kanuni za bunge, Siku ambayo mwezetu ameondoka duniani, tunakua hatuna bunge. Kutokana na kifo hicho basi, Bunge linaahirishwa hadi kesho saa tatu Asubuhi. Kwa wale Wabunge watakao takiwa kwenda kuzika, Ofisi ya katibu inaendelea kufanya utaratibu
 
Jaman ... Poleni wanainchi wa Geita na Wanachama Wa Chama Cha Mapinduzi..

ila uthibitisho Wa Hizi taarifa unahitajika
 
ladies and gentlemen

we a Mourning the death of Geita MP Donald
Max. He is 8th to depart. Others are
Mwaiposa, Komba, Sumari, Mtema, Khamis,
Mgimwa & Bwanamdogo.

May his soul rest in peace! !!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom