Tanzia: Matwi afiwa na baba yake mzazi

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
UPDATES.
Kwa niaba ya familia yake Matwi ametoa shukrani nyingi kwa wote waliofanikisha mazishi ya marehemu baba yake kwa njia moja ama nyingine. Anasema amefarijika sana.

Taarifa kutoka kwa wafiwa, ni kuwa mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu (17.10.2011). Ibada ya kumwombea marehemu itaanza kuanzia saa sita na ni tumaini letu hadi saa nane kila kitu kitakuwa kimekamilika. Ombi, tunaomba wanaJF wote walio Arusha wajitahidi kudhuria mazishi hayo ili tuonyeshe mshikamano wetu kivitendo.

Wana JF member mwenzetu aitwaye Matwi amefiwa na baba yake mzazi jana (13.10.2011). Msiba upo NAIC Usa - Arusha. Kifo cha marehemu kimesababishwa na ajali gari, yaani aligongwa na hiace. Mara kikao cha familia kitakapokaa mtajulishwa ni lini mazishi yatafanyika na wapi. WanaJF wa Arusha natumaini wengi wenu mtakuwa mlishatumiwa message ya taarifa ya msiba huu, hivyo mnahitajika kuwa flexible pindi tutakapopata taarifa ya lini mazishi yatafanyika. Aidha ni imani yetu kuwa wapo wana JF wengi ambao hawatambui uwepo wa umoja wa wanaJF Arusha, hivyo tunawasihi nao wajitokeze kwa wingi baada ya kupata updates kupitia thread hii au wanaweza kumPM PakaJimmy au Mzee wa Rula kwa habari zaidi. Kwa niaba ya wanaJF Arusha napenda kutoa pole kwa familia ya marehemu, tunasema BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
 
Mkuu poleni,

Salamu za pole ziwafikie wanafamilia wote, bwana alitoa na bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. Ameni
 
Poleni wafiwa. Mungu awape uwezo wa kukabiliana na maisha mapya.
 
Pole kwa familia ya marehemu. Tunawaombea mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu walichonacho.
RIP baba Matwi.
 
Pole sana kamanda.....ni moja ya safari katika maisha....Mungu amlaze baba mahali pema peponi....Amen
 
pole kamanda.. Niko hapa nje kwenu naota moto.. We loved him but God loved him the most
 
Ni kweli katika maisha nadhani hakuna msiba mzito kama wa kuondokewa na mzazi, Mungu aipe uvumilivu familia katika kipindi hiki kigumu.

yep kaka, kuna wengine huweza kuvumilia, ila nguvu za ziada zinahitajika ili kukabili hali yenyewe!
 
yep kaka, kuna wengine huweza kuvumilia, ila nguvu za ziada zinahitajika ili kukabili hali yenyewe!
Ndiyo hivyo mkuu, kufiwa hakuzoeleki kabisa. Tuombe Mungu familia itambue baba yao yupo katika pumziko la milele ambako sote tutapita wakati ukifika. Hii itawapunguzia uzito wa msiba kidogo.
 
Back
Top Bottom