Tanzia: Matwi afiwa na baba yake mzazi

Nasikitika sana kupata taarifa hizi ambazo ni mbaya sana!
Mkuu Matwi, we ni mwanaume, kaza moyo, ndiyo ya dunia!
Naamini kuwa unamjua Mungu, na una tumaini la uzima wa milele!
Basi kama ndivyo, amini kuwa baba yu hai kiroho, na ipo siku utakuwa naye pamoja!
Pole sana kiongozi, tupo pamoja.
 
Poleni sana Kamanda wewe na Familia yako.
Mungu awape moyo wa subira na kwa Marehemu ninamuomba Malazi Mema!
 
Nasikitika sana kupata taarifa hizi ambazo ni mbaya sana!
Mkuu Matwi, we ni mwanaume, kaza moyo, ndiyo ya dunia!
Naamini kuwa unamjua Mungu, na una tumaini la uzima wa milele!
Basi kama ndivyo, amini kuwa baba yu hai kiroho, na ipo siku utakuwa naye pamoja!
Pole sana kiongozi, tupo pamoja.
Ni kweli PJ, "Basi kama ndivyo, amini kuwa baba yu hai kiroho, na ipo siku utakuwa naye pamoja!"
 
asanteni wote na endeleeni kuniombea kwani niwakati mgumu ninaopitia ukichangia ni mtoto wa kwanza katika familia

Pole mkuu, jipe moyo na tuko pamoja. Naomba details za namna ya kufika hapo Usa. Unashuka wapi na unaelekea upande gani na vitambulisho muhimu kama vile ni mtaa gani, kuna kanisa au msikiti gani karibu, au mtu maarufu wa kumuulizia ili kufika nyumbani kwako.
 
Wengine ndo tuko njiani kuelekea Arusha, Nasahauri (kama halipo) liandaliwe daftari la JF MEMBERS ONLY hapo msibani ili wadau wakifika hapo wanatoa rambirambi zao humo, hii itasaidia kufahamu JF members tulioshiriki and the way forward baada ya msiba.
 
Sidhani kama lipo ila Arusha tuna umoja wa wanaJF na kila mwanachama anapopatwa na matatizo yaliyoainishwa katika katiba basi hupewa Tshs 200,000.00 kwa sasa kama pole. Hivyo wanaJF walio katika umoja huo wanakuwa at least kila mmoja amemchangia mwenzake katika tatizo hilo. Lakini wale ambao hawajui hakuna shida tunaweza kuwasiliana aidha kupitia PakaJimmy au Mzee wa Rula ili kuongeza ubani ili tukitoa ubani wetu i sound kama wanaJF wote. Hii ni kuepuka kila mtu kwenda kumpa pole au rambirambi kivyake au binafsi japokuwa haikatazwi. Nadhani utakuwa umenipata.
 
asanteni wote na endeleeni kuniombea kwani niwakati mgumu ninaopitia ukichangia ni mtoto wa kwanza katika familia

Kamanda!! Nazidi kukutakia pole nyingi sana nimeona machungu makubwa yaliyokugusa pamoja na familia yenu. Ila hakika ninafarijika sana kwani hakika yupo MTETESI wa yote na atasimama na atatetea watokao Kusini na hata Kaskazini,Kamanda piga moyo kondo na hakika tutafika tu. UWE NA WAKATI MZURI!
 
Jana baadhi ya WanaJF waliopata nafasi tulihidhuria mazishi ya baba ya mwenzetu Matwi. Kifupi hana mengi ya kusema zaidi ya haya, "Kwa niaba ya familia yangu natoa shukrani nyingi kwa wote waliofanikisha mazishi ya marehemu baba yake kwa njia moja ama nyingine.Nimefarijika sana, Mungu awazidishie sana jamani. Sina cha kuwalipa zaidi neno Asante kwa yote mliyonifanyia"
 
jana baadhi ya wanajf waliopata nafasi tulihidhuria mazishi ya baba ya mwenzetu matwi. Kifupi hana mengi ya kusema zaidi ya haya, "kwa niaba ya familia yangu nametoa shukrani nyingi kwa wote waliofanikisha mazishi ya marehemu baba yake kwa njia moja ama nyingine.nimefarijika sana, mungu awazidishie sana jamani. Sina cha kuwalipa zaidi neno asante kwa yote mliyonifanyia"

tupo pamoja kamanda wetu.
 
Jana baadhi ya WanaJF waliopata nafasi tulihidhuria mazishi ya baba ya mwenzetu Matwi. Kifupi hana mengi ya kusema zaidi ya haya, "Kwa niaba ya familia yangu natoa shukrani nyingi kwa wote waliofanikisha mazishi ya marehemu baba yake kwa njia moja ama nyingine.Nimefarijika sana, Mungu awazidishie sana jamani. Sina cha kuwalipa zaidi neno Asante kwa yote mliyonifanyia"

kila la kheri.
 
Nilifanikiwa pia kuwepo mazishini, the situation was so tense to our friend, but God helped us to a bit comfort him!
 
kama alivyo kwisha sema mzee wa rula,Kwa niaba ya familia tuna shukuru sana kwa michango yenu ya hali na mali,maombezi yenu kwa ujumla ninashukuru sana.
Pia nawashukuru wote mlioweza fika katika msiba na wale wote ambao hawakuweza kufika ila kiroho walikua nasi,nashukuru sana kwani uwepo weno ulinifariji sana sana..
Mzee wetu ametutoka kimwili ila kiroho yu nasi.Bwana ametoa bwana ametwaa.Jina lake lihimidiwe
Narudia tena asanteni sana wote na mbarikiwe wote.Tuendeleee na majukumu ya kujenga Taifa letu.
Mungu endelea kuibariki Tanzania
 
kama alivyo kwisha sema mzee wa rula,Kwa niaba ya familia tuna shukuru sana kwa michango yenu ya hali na mali,maombezi yenu kwa ujumla ninashukuru sana.
Pia nawashukuru wote mlioweza fika katika msiba na wale wote ambao hawakuweza kufika ila kiroho walikua nasi,nashukuru sana kwani,,,,,,a uwepo weno ulinifariji sana sana..
Mzee wetu ametutoka kimwili ila kiroho yu nasi.Bwana ametoa bwana ametwaa.Jina lake lihimidiwe
Narudia tena asanteni sana wote na mbarikiwe wote.Tuendeleee na majukumu ya kujenga Taifa letu.
Mungu endelea kuibariki Tanzania

Best! Bado nasema pole sana tena sana,kwani Baba ametutoka kimwili ila hakika kiroho tu pamoja. UWE NA WAKATI MZURI NA WA AFYA NJEMA.
 
Back
Top Bottom