TANZIA Makongoro Mahanga afariki dunia asubuhi ya leo Muhimbili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
TANZIA: MWENYEKITI WA CHADEMA ILALA AFARIKI DUNIA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Ilala, Dk Milton Makongoro Mahanga amefariki dunia wakati anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Hemed Ally amethibitisha hilo. Taratibu na taarifa zaidi zitafuata

IMG_20200323_083308_752.jpg
WASIFU WAKE KWA UFUPI

Dk. Milton Makongoro Mahanga ni mwanasiasa ambaye amekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM na baadaye Segerea kwa jumla ya miaka 14 kuanzia mwaka 2000, na Naibu Waziri wa Miundombinu na baadaye Kazi na Ajira kwa jumla ya miaka 9 kuanzia mwaka 2006.

Jumapili Agosti 2, 2015 akiwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea, Mhe. Dkt. Makongoro Milton Mahanga alitangaza kujiondoa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Ailizaliwa katika kijiji cha Mugeta wilaya ya Mara Kusini (sasa Bunda) tarehe 3 Aprili 1955. Alipewa jina la Makongoro ambaye alikuwa Chifu wa Waikizu ingawa asili yake ni wilaya ya Mara Kaskazini (sasa Rorya).

Alisoma katika Shule za Msingi za Kyambai (sasa Matare) na Mugumu katika wilaya hiyo ya Serengeti na Bukama Ikizu katika wilaya ya Bunda kati ya mwaka 1965 na 1971. Mwaka 1972 hadi 1975 alisoma kidato cha Kwanza hadi cha Nnne katika Shule ya Sekondari Mara na baadaye kumaliza masomo ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam.

Kuanzia mwaka 1978 hadi 1980 alichukua masomo ya Shahada ya Kodi na Uhasibu katika Chuo cha Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam. Kupitia Bodi ya Ununuzi na Ugavi ya NBMM (sasa PSPTB) alikuwa Mtanzania wa kwanza kupata Stashahada ya Juu ya Ununuzi na Ugavi CSP (sasa CPSP) inayotolewa na NBMM mwezi Mei 1980. Aidha kwa mara nyingine alikuwa Mtanzania wa Kwanza kuwa na CSP na CPA kwa pamoja pale alipofanikiwa kupata Stashahada ya CPA inayotolewa na Bodi ya Uhasibu (NBAA) mwezi Mei 1983.

Baadaye Makongoro alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), alijiendeleza kusoma na kutunukiwa cheti cha uzamili kwenye masuala ya fedha (MSc Finance) mwaka 1997 kupitia Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Glasgow nchini Uingereza.

Aidha kupitia utafiti wa kina alioufanya nchini Tanzania na nchi nyingine kama Uingereza, Kenya na Uganda kuhusu mahusiano kati ya umasikini na makazi duni mijini, alifanikiwa kutunukiwa Shahada ya uzamivu (PhD) kupitia Chuo cha Washington International University cha nchini Marekani Julai mwaka 2000. Kwa umahiri wake, utafiti wake huo uliweza kuchapishwa mwaka 2002 na wachapishaji wa Dar es Salaam University Press (DUP) kama kitabu: "Urban Housing and Poverty Alleviation in Tanzania" kwa namba ISBN 9976-60-343-6.

Pia alifanya kazi katika Idara ya Kodi ya Mauzo (Sales Tax Department) Wizara ya Fedha katika Ofisi ya Kodi Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1977 hadi 1980.

Aidha alifundisha masomo ya ununuzi na ugavi (kwa miaka 14) na kutunga na kuandika vijitabu zaidi ya vinne kwenye fani hii,. Lakini pia alichangia sana kuendeleza Bodi ya taaluma ya ununuzi na ugavi nchini (NBMM) kama mtaalamu, mjumbe na Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa jumla ya miaka 25. Lakini pia alishiriki katika uanzishwaji na uendelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (PPA) hapa nchini kama mtaalamu wa fani hii.

Wakati akimaliza CSP mwaka 1980 tayari alishamaliza cheti na diploma ya uhasibu (NABOCE na NAD) na ilipofika Mei 1983 alitunukiwa stashahada ya CPA na Bodi ya NBAA na hivyo akaweka tena historia nchini kwa kuwa mtanzania wa kwanza kuwa na CSP na CPA kwa pamoja. Kwa kuwa alikuwa tayari ni mtaalamu aliyeidhinishwa kwenye fani ya Ugavi na Uhasibu (Certified Supplies Professioinal na Certified Public Accountant), baada ya kuacha kufundisha Nyegezi, mashirika yote aliyofanya kazi aliongoza idara zilizokuwa zinasimamia masuala ya fedha na pia masuala ya ununuzi na ugavi.

Kwa miaka sita (1985-1991) alikuwa Mhasibu Mkuu wa Bima Motors alisimamia pia Idara ya Ununuzi na Ugavi. Mwaka 1991 hadi 1994 alikuwa Msarifu (Bursar) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiongoza Idara za Fedha na pia idara ya Ununuzi na Ugavi, na kwa miaka sita (1994 hadi 2000) alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akisimamia pia Idara ya Ununuzi na Ugavi.

Alipoingia Chuo Kikuu cha UDSM mwaka 1991 alikuta mahesabu ya Chuo hicho yakiwa hayajakaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa miaka karibu 10.

Kwa muda wa miaka minne tu aliyoongoza Idara ya Fedha na Ugavi kama Msarifu, mahesabu yote hayo yalikaguliwa na hatimaye mahesabu ya mwisho kupata hati safi.

Hivyo nilipoingia NHC mwaka 1994, nilikuta mahesabu ya shirika yako nyuma toka Shirika la Msajili wa Majumba na Shirika la Nyumba yaungane mwaka 1990. Kwa usimamizi wangu, mahesabu yote ya nyuma yalikaguliwa na wakati natoka NHC kugombea ubunge mwaka 2000, CAG alikuwa amekamilisha ukaguzi wa hesabu za NHC za mwaka 1999 na zilipata hati safi.
 
RIP makongoro mahanga


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom