TANZIA: Kocha na mchezaji wa zamani wa Nigeria Stephen Keshi afariki ghafla

fungi

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,539
4,668
Mchezaji wa zamani wa Nigeria Stephen O. Keshi a.k.a the Boss amekufa ghafla kwa shambulio la moyo.

Kwa maelezo ya wanafamilia na marafiki wa karibu kocha huyo wa zaman wa super eagles hakuonyesha dalili zozote za kuumwa.
Alikuwa akiishi na mama yake na watoto wake wa nne

Keshi ni kocha pekee mzawa wa Nigeria kushinda Afcon mwaka 2013.
R.I.P Legend

1465362281043.jpg
 
Nahodha na kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Nigeria "Super Eagles" Steven Keshi amefariki leo huko kwao Nigeria
image.jpeg
 
Aaaiiiiiyaaaaaaaaa!!!!!!

Daah, kunakipindi fulani Azam walijaribu kumfukuzia awe kocha wao baada ya kutimuliwa Kocha wao aliyepita.

So sad ktk jamii ya wapenda soka, Familia yake na Nchi yake kwa Ujumla.

Nwanko Kanu atalia sana juu ya kifo hiki. Maana kaanzisha Hospitali maalumu kwa Magonjwa ya Moyo hapo Nigeria na Rafiki, Mchezaji, kocha na Mwananchi mwenzake kafa kwa Ugonjwa huohuo, Inauma sana.

Raha ya Milele umpe ee Bwana, Na mwanga wa milele umwangazie, Apumzike kwa Amani.Amina

BACK TANGANYIKA
 
pole sana wapenzi wa soka. Alikuwa anawindwa na Azamu ya Tanzania nami nilidhani ipo siku atakuja kufundisha timu Tanzania. R.I.P
 
Hii timu ya Nigeria ya mwaka 1994 ilikuwa kiboko na ni Emanuel Amunike na Oliha Thompson pekee ndio waliokuwa wametoka kwenye timu za Afrika, waiobakia walikuwa ni wataalam.

Nakumbuka niliangalia mechi hii na marehemu Keshi aliongoza safu yake ya ulinzi kwa uadilifu kabisa.

Nigeria lishinda kombe la mataifa ya Afrika na baadae akaja kushinda na Nigeria akiwa meneja wao.

Marehemu Stephen Keshi amewahi pia kuwa meneja wa timu za taifa za Mali naTogo.

Ni mmoja wa walimu wa mpira na wachezaji wa zamani waliocheza mpira wauhakika barani Ulaya, walioheshimwa sana.


1 GK Peter Rufai Go Ahead Eagles (NED)
2 DF Augustine Eguavoen Kortrijk (BEL)
3 DF Benedict Iroha Vitesse Arnhem (NED)
4 DF Stephen Keshi Molenbeek (BEL)
5 DF Uche Okechukwu Fenerbahce (TUR)
6 DF Chidi Nwanu RSC Anderlecht (BEL)
7 FW Finidi George Ajax (NED)
8 MD Oliha Thompson - Africa Sports (CIV)
9 FW Rashidi Yekini - Vitoria Setubal (POR)
10 MD Augustine Okocha - Eintracht Frankfurt (GER)
11 FW Emmanuel Amunike - Zamalek (EGY)
12 MD Samson Siasia- Nantes (FRA)
13 DF Emeka Ezeugo - Honved (HUN)
14 FW Daniel Amokachi -Club Brügge (BEL)
15 MD Sunday Oliseh - RC Liege (BEL)
16 GK Alloysius Agu -RC Liege (BEL)
17 FW Victor Ikpeba -AS Monaco (FRA)
18 FW Efan Ekoku - Norwich City (ENG)
19 DF Michael Emenalo- (no club)
20 FW Uche Okafor - Hannover 96 (GER)
21 MD Mutiu Adepoju - Racing Santander (SPA)
22 GK Wilfred Agbonavbare -Rayo Vallecano (SPA)

Nimejifunza kitu fulani hapa.

RIP Stephen Keshi.
 
Back
Top Bottom