TANZIA: Kamanda wa polisi wa zamani Kilimanjaro, Dr. Mohammed Chico afariki dunia

Bollo Yang

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
440
50
Imetokea asubuhi hii, Mazishi yatafanyika leo saa kumi jion katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.

========
Chico.png

Kamanda wa polisi wa zamani mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Mohamed Chico amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salam.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia Bw. Awadhi Chico, mazishi yake yamepangwa kufanyika leo Jumapili 22/01/2017 jioni katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kijitonyama.

RIP kamanda Mohammed Chico, Inna lillaah wainnaa ilayhi raajiuun
 
RIP...Polen sana ila ungefafanua zaidi mkuu kamanda Chico alikuwa nani sio wote tunamfaham..
Wengine humu huwa tunasahau kwamba kuna vijana waliozaliwa miaka ya 2000. Mara nyingi huwa tunadhani wote ni wa miaka ya 60, 70 na 80. Kamanda Chico alikuwa ni RPC na mara ya mwisho alikuwa RPC Kilimanjaro kabla hajahamishiwa makao makuu ya polisi na kustaafia Makao Makuu ya Polisi. Alikuwa kamanda maarufu kwa mambo mbalimbali. Sijui kama yote yalikuwa na ukweli ama la.
RIP kamanda Chico.
 
Polen sana wafiwa
Lakini ni kwa nini mabosi wanapojiuzulu au kuachishwa kazi wengi huaga dunia mapema?? Kuna nini hasa?
 
Back
Top Bottom