Tanzia: KakaKiiza (JF Member) afiwa na Mkewe!

Pole sana KakaKiiza na familia nzima kwa msiba huu mkubwa. Tunakuombea kwa Mungu Akupe nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu.
Mungu Ampumzishe mpendwa wetu mahali pema!
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe!
 
Pole sana mkuu KakaKiiza kwa kuondokewa na mkeo mpendwa. Nakuombea kwa Mungu akupe faraja na moyo wa subra katika kipindi hiki cha maombolezo.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana KakaKiiza! Mungu akutie nguvu na kukupa faraja ya pekee katika kipindi hiki kigumu! Poleni sana!
 
maskini kaenda akiwa mjamzito, nimeumia zaidi, i can imagine the pain she felt, MUNGU MWEMA AMSAMEHE MAKOSA YAKE NA IMPENDEZE KUMPOKEA KWAKE MBINGUNI, AMEN!
 
Pole sana KakaKiiza Mwenyezi Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Raha ya milele ampe ee bwana na mwanga wa milele amuangazie, apumzike kwa amani....Amina.
 
Last edited by a moderator:
May her soul rest in peace......Amen! Pole sana KakaKiiza pamoja na wafiwa wengine wote, Mwenyezi Mungu awatie mioyo ya faraja!
 
pole sana mwanajamvi mwenzetu, Mungu akutumie msaada toka patakatifu pake na akupe faraja itokayo kwake. Jina la Bwana libarikiwe.
 
Sisi sote ni wa Mwenye ez Mungu na kwake ndio marejeo yetu, pole wafiwa Mola atawajaalia faraja Amin.
 
Pole sana Kakakiiza na familia yako kwa ujumla Inasikitisha sana mpaka mwili umesisimka kwa wogahaya matatizo ya uzazi jamani mungu atusaidie."Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe."Mungu awape moyo wa subira na ujasiri katika kipindi hiki kigumuAmen.
 
Inna Lillah Waina Illahi Rajoon
Sisi ni wa Mwenyezi-Mungu nasi sote Kwake tutarejea.


Pole sana mkuu, Mwenyezi-Mungu akupe subra katika kipindi iki kigumu.
 
Pole sana Kaka,

Na RIP Shemeji yetu....

Kifo cha ujauzito ni kifo kitakatifu. Naamini Mungu atampa marehemu upendeleo wa pekee katika makao yake Mbinguni kwani katoa uhai wake katika mchakato wa kuleta uhai kwa kiumbe kipya!!

Raha ya milele ampe ee Bwana, na Mwanga wa milele amwangazie...Apumzike kwa amani!!
 
Pole sana Kaka Kiiza. Pumzika kwa Amani Mrs Kiiza, tuliumbwa kwa udongo na udongoni tutarudi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom