Tanzia: KakaKiiza (JF Member) afiwa na Mkewe!

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
Wana Bodi,

Nasikitika sana kuwapa taarifa za msiba wa Mke wake na Kaka Kiiza, kilichotokea sasa hivi. Nimepata ujumbe wake kwa njia ya sms juu ya taarifa hizi za kusikitisha.

Naungana na ndugu na jamaa wa ndugu yetu katika maombolezo ya msiba huu mkubwa.

Kaka Kiiza, Asured kwamba mawazo yetu na sala zetu yapo na nawe katika kipindi hiki chote cha msiba! Jipe Moyo Mkuu kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa hata kidogo...

Binafsi sikupata details zaidi!! nitakapopata nitaziweeka hapa


Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Libarikiwe!

Kwa wale watakao weza kuhudhuria msiba safadhali tukamtie mwenzetu Moyo!

Kiresua

More info!!

Mama Kiiza amefikwa na mauti kwa sababu za ujauzito!

Updates...

Wapendwa Leo heshima za mwisho zitatolewa Tegeta Namanga saa 7-8Mchna na baada ya hapo msafara utaanza kuelekea Makaburini kinondoni,makaburi ya karibu na Hananasif!Mwembeni karibu na njia ya kwenda leaders club!
 
Mkuu kiiza pole sana nakutakia moyo mkuu katika kipindi hiki kigumu!
R.I.P Mama Kiiza
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Pole sana Mkuu,Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu sana.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Poleni sana wafiwa. Mungu awape nguvu katika wakati huu mgumu kwenu.
R.I.P Shemeji
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Nasikitika kuwataarifu kuwa mwanachama mwenzetu wa hapa JF ambaye pia ni mwanachama wa JE Saccos ndugu KakaKiiza amefiwa na mke wake takribani dakika 40 zilizopita kwa mujibu wa maongezi mafupi na mfiwa, marehemu amekutwa na mauti akiwa na ujauzito.

Kama mwanachama mwenzetu wa JF nampa pole sana mwenzetu na natoa wito tumpe sapoti kadri inavyowezekana na inapowezekana msiba upo TEGETA NAMANGA KWA MAJURA

Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho Ya Marehemu. Amina
 
Last edited by a moderator:
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom