TANZIA Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu, Upendo Msuya afariki dunia

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Nasikitika kuwaarifu kuwa Mhe Jaji Upendo Msuya,(rtd) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Kairuki. Hakika sisi sote ni wa Mungu na kwake yeye tutarejea.

=======
Msuya.png

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ambaye amejiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya amefariki leo Julai 19 baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, mjomba wa marehemu, Niva Mbaga amesema kwamba marehemu amefariki akiwa Hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa.

Amesema kwamba shughuli za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tegeta jijini Dar es Salaam.

“Amesumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi hivyo akawa anapelekwa hospitali na kurudi nyumbani zaidi ya miezi mitatu sasa na leo hii amefariki dunia’’ amesema Mbaga

Amesema marehemu ameacha watoto wanne.

June 2008, aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, alimteua Upendo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nafasi ambayo ameitumikia hadi May 2017 alipojiuzulu.

DFFLXmcXoAAD-IM.jpg:large.jpeg

Mada inayomhusu Jaji Msuya
RC wa Kilimanjaro, Meck Sadiki na Majaji wawili Wajiuzulu. Rais Magufuli aridhia...
 
Pole kwa familia yake... Ameshamaliza safari yake alale pema tupo tunakuja
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Tunaposema RIP mara nyingi twakosea, mtu akifa amekufa hajui chochote kinachoendelea duniani

Zaidi tutoe pole kwa familia yake na ndugu zake na watu waliokuwa karibu naye
Roho ya mtu haifi ila humrudia Yeye aliyeitoa..

Kwa Wakristo

Mhubiri 12:7
[7]Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa,
Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
 
Back
Top Bottom