TANZIA TANZIA: Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani afariki dunia

Angalia hapa, kwa utaratibu mzuri katika wikipedia:

Augustino S.L. Ramadhani (28.12.1945 - 28.04. 2020) alikuwa mwanasheria. mwanajeshi na mwanatheolojia kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alijulikana kwa huduma yake akiwa Jaji Mkuu wa Tanzania, baadaye pia katika Tume ya Uchaguzi na Zume ya Katiba.


Yaliyomo
Maisha binafsi
Ramadhani alizaliwa mjini Zanzibar, mtaa wa Kisima Majongoo, katika familia ya kikristo ya dhehebu la Kianglikana akiwa mtoto wa pili kati ya wanne wa mwalimu Mathew Douglas Ramadhani na mkewe Bridget Anna Constance Masoud. Mwaka 1952 familia ilimfuata baba aliyehamishwa kufundisha pale Mpwapwa, baadaye Tabora na tena Mpwapwa. Mtoto Augustino alisoma elimu ya msingi hadi 1959 kwenye shule mbalimbali mahali babake alipofanya kazi. 1960 alipokelewa katika shule ya sekondari "Tabora Boys" alipohitimu mwaka 1965 baada ya kumaliza kidato cha sita. Katika kipindi hiki alipokea taarifa ya kifo cha babake alifariki katika ajali nchini Uingereza alipokwenda kusoma. Agustino alikumbukwa Tabora kama mwanariadha wa mpira wa kikapu na pia mpiga kinanda.

Baada ya kumaliza masomo cha Chuo Kikuu na kujiunga na jeshi alimwoa Saada Mbarouk akazaa naye watoto wanne, ambao wawili ni wavulana Francis na Mathew na wawili ni wasichana Marina na Bridget.

Masomo
Baada ya kuhitimu kidato cha sita alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akasoma fani ya sheria akafikia shahada ya awali mwaka 1970. Katika kipindi hiki alikata kadi ya uanachama wa chama cha TANU. Alikuwa kati ya wanafunzi waliofukuzwa na rais Nyerere mwaka 1966 baada ya kugoma na kuruhusiwa kurudi 1967.

Maishani mwake alirudi chuoni mara mbili pamoja na kazi mbalimbali, 1978 alipata shahada ya uzamili Dar es Salaam katika Sheria za Kimataifa. 2004 alisoma theolojia kwenye Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza alipopata shahada ya kwanza ya uchungaji (Bachelor of Divinity).

Mwanasheria jeshini
Mwaka 1970, baada ya kumaliza Chuo Kikuu, aliingia katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akawa na cheo cha kijeshi hadi 1997. Baada ya kupata mafunzo katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania alipandishwa cheo kama Luteni wa Pili. 1978 alipelekwa Zanzibar kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. 1979 alihitajika tena jeshini akiongoza mahakama ya kijeshi katika Vita vya Kagera akipandishwa cheo hadi Luteni Kanali. 1997 alistaafu rasmi jeshini akiwa na cheo cha Brigedia Jenerali.

Jaji Mkuu Zanzibar
1980 aliitwa tena kuja Zanzibar na kuwa Jaji Mkuu, kazi aliyofanya hadi mwaka 1989. Alibadilisha mfumo wa mahakama visiwani uliofuata bado mitindo ya mapinduzi ambako watu raia, wasio na elimu ya kisheria, waliangalia kesi katika mabaraza ya wananchi. Ramadhani aliunda mfumo wa ngazi za kimahakama hadi Mahakama ya Rufaa.

Mahakama ya Rufaa na Tume ya Uchaguzi
1989 aliteuliwa na rais Ali Hassan Mwinyi kuwa jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania. 1993 alipewa kazi ya nyongeza akiitwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Alihudumu kwenye cheo hicho hadi mwaka 2003.

Vilevile aliteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki kwenye Novemba 2001 akihudumu hapa hadi mwaka 2007.

2002 alichaguliwa pia kuwa Makamu wa Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi, Zanzibar (ZEC) hadi 2007.

Jaji Mkuu wa Tanzania
2007 aliteuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania. Aliondoka katika kazi hiyo mwaka 2010 baada ya kufikisha miaka 65, ambao ni umri wa kisheria kwa majaji wa Tanzania.

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu
Baada ya kipindi cha Jaji Mkuu alikubali kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu alichofanya kuanzia 2010 hadi 2016. Tarehe 14.9.2014 alichaguliwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu akipata kura 9 dhidi ya 4 kwa mpinzani wake.

Mchungaji wa Kanisa Anglikana Zanzibar
Mwaka 2013 alikubali ombi la askofu wa Dayosisi ya Zanzibar akaingia katika utumishi wa Kanisa Anglikana kwenye ngazi ya ushemasi kwa nusu mwaka halafu alitawazwa kuwa kasisi wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Zanzibar baada ya kuwa Shemasi kwa miezi sita. Mchungaji AUGUSTINO alitawazwa katika ibada mjini Zanzibar, Unguja tarehe 28.12.2013.

Wakati ule alifundisha pia sheria katika Chuo cha Tumaini Iringa.



Siasa
Ramadhani alikuwa mwanachama wa TANU na baadaye CCM tangu siku zake za mwanafunzi kwenye chuo kikuu. Mwaka 1996 alirudisha kadi yake ya uanachama kufuatana na kanuni za katiba iliyobadilishwa kuwa majaji na wanajeshi wa Tanzania wasiwe wanachama wa chama cha kisiasa. Baada ya kustaafu katika utumishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alirudi CCM kwenye mwaka 2011.

2015 Ramadhani alijaza fomu ya kuwa mgombea wa urais kwa CCM, lakini hakuteuliwa na chama.



Maandiko
Amechapisha makala kuhusu Haki za Binadamu, kama vile, miongoni mwa nyingine, 'Kukuza Agizo Jipya la Uchumi katika Kuendeleza Nchi: Jukumu la Asasi za Haki za Binadamu', iliyochapishwa katika Kuzungumza juu ya Haki (jarida la msingi la haki za binadamu la Canada), Vol. XI No. 3/1996, na Mchakato wa Uchaguzi katika Demokrasia ya Multiparty, sura katika kitabu cha Haki za Binadamu na Ukombozi nchini Tanzania, (Mkuki na Nyota Publishers, 1978).


Marejeo
Augustino Ramadhani - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
When you test positive to COVID19, just know you're in trouble, coz they will need all contacts including all girlfriends/ and boyfriends, will know which lodge you stayed, who you paid to, who served you food and drinks and when you checked out.

I have never seen a virus that embarrasses people like this one
Ni balaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom