TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Ooh my good!
Mungu aitwe mungu mungu usiyepangiwa mungu usietabiriwa mungu usiefundishwa Bali ni mungu atandae linalompendeza,
Deo we loves u but god loves u more
Rest in peace deo
 
Deo jmn, deo jmn, deo jmn tunakulilia, mimi ni Ukawa ila nilikua nakuadmire sana, km ni kweli pumzika kwa amani
 
Hapa kuna kitu si bure ..serikali ifanye kazi tusije kidharau mwiba mguu ukaota tende ..kwanini sahivi? kwanini watu fulani wenye hoja fulani?
 
14353341 said:
Nchi ya ajabu sana hii badala ya kufa mafisadi wanakufa watetezi wa wananchi.!

RIP Filikunjombe.

idawa wote tumeshtushwa sana na msiba huu wa Deo hivyo anaepanga kifo ni Mungu ndo huamua kwa wakati wake hivyo hili tumwachie Mungu ndo ajuae hujawahi ona hata kwenye familia waweza kuta yule mtu mzuri mwenye Upendo na wenzie ama mwenye kitu ambacho wengine hawana anakufa mapema anawaacha mwenye roho mbaya yote ni mipango ya Mungu
 
Poleni wafiwa wote. KIfo cha Deo Filikunjombe ni pigo kubwa si kwa Ludewa pekee wala CCM, bali ni kwa Taifa zima. Deo alijipambanua kama mwanasiasa kijana aliyeweka mbele maslahi ya nchi, tofauti na wanasiasa wengine ambao kwao vyama ni zaidi ya nchi. Mara ya mwisho tulionana na kuaungumza na Deo katika hoteli ya St, Gasper, Dodoma. Hatuna la kufanya isipokuwa kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Jamani Deo, Filikunjombe wewe nalia mimi.
Ulikuwa mwadilifu sana, may his soul rest in peace.
 
wakuu,ningependa kujualishwa hizi chopa ccm wanazotumia ziko ngapi?na uhuru kenyatta amegawa bure au zimekodiwa.
asanteni
 
Kwa habari nilizozipata hivi punde ni kwamba aliyekuwa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe amefariki dunia katika ajali ya helikopta iliyoanguka huko mbuga za selous Morogoro. Mwenye taarifa zaidi kuhusu tukio hilo naomba atujuze.
 
Hii ni nouma, sitaki kuwa mpiga ramli ila huu uchaguzi upite tu, nahisi giza nene ndani ya Nchi.
 
daaah! deo tena!! alikuwa na msimamo dhabiti! ccm pgo kubwa,hlo jmbo upnzan tusingepata! R.I.P deo na wenzako!
 
Back
Top Bottom