dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Mwimbaji gwiji wa muziki wa TAARAB asilia kutoka Zanzibar wa kundi maarufu duniani lenye miaka zaidi ya 105 Nadii Ikhwaan Safaa (Malindi Musical Club), Bi Fauzia Abdallah, amefariki dunia hospitali ya Muhimbili alfajiri ya Mei 11.
Bi Fauzia alitamba sana katika miaka ya 1980 akiwa na kundi hilo la Malindi Musical Taraab na nyimbo zake nyingi "Lishalo Limekwisha" na “Nimesalitika”.
Pia bi Fauzia alikuwa mke wa mtunzi mahiri na mpiga qanoun Ally Salum Bassallama wa kundi hilo maarufu ambalo ndilo kundi la mwanzo la taarab barani Afrika lililoanzishwa mwaka 1905 huko Zanzibar.
Bi Fauzia amefariki katika wodi ya Kibasila alikokuwa akipata matibabu ya saratani.
Marehemu ya Bi Fauzi ambaye ameacha watoto watatu, mazishi yamefanyika huko Zanzibar.
Mola amlaze mahala pema peponi amen.