TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde

Mtangazaji maarufu Ephraim Kibonde amefiwa na mkewe usiku huu katika hospitali ya Hindu Mandal. Bwana ametoa Bwana ametwaa. Amen.

======

Mke wa Mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde amefariki.
View attachment 806825
Kwa mujibu wa Mtangazaji mwenzie Gadner G. Habash amesema Mke wa Kibonde aitwae Sara Kibonde amefariki usiku huu akiwa anapatiwa matibabu ktk hospitali ya Hindu Mandal. R.I.P
Kila nafsi itaonja umauti- hii ni njia yetu sote yeye ametangulia tu "RIP"
 
Pole sana Kaka yangu na Kiongozi wangu wa Kitaaluma pia Ephraim Kibonde kwa Kuondokewa na Mpendwa Mke wako Sarah. Binafsi naungana nawe katika Kipindi hiki Kigumu na namwomba Mwenyezi Mungu akutie nguvu, akupe rehema na uvumilivu pia. Kikubwa tumshukuru Mwenyezi Mungu na tumuombee sana Mpendwa wetu Sarah ili apokelewe vyema huko aendako.

Nimepokea taarifa hii kwa mshtuko mkubwa mno, najua maumivu uliyonayo Kaka ila jikaze na yote tumshukuru Maulana.
nilijua tu kwenye huu uzi huwezi kosekana hapa
 
Back
Top Bottom