Tanzia: Dr. Sengondo Mvungi afariki Dunia

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
811
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid leo jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.

"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali.

"Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa kesho (Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza.

Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.

Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.

CHADEMA WATOA RAMBIRAMBI
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametuma salaam za rambirambi ya kifo cha Dkt. Edmund Sengondo Mvungi, akitoa pole kwa familia, uongozi na wanachama wa NCCR-Mageuzi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya na wananchi wote walioguswa na msiba huo.

Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wa chama hicho, Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa amepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa za kifo cha Dkt. Mvungi, akimwelezea kuwa alikuwa mwanasiasa mwenye msimamo ambaye hakuwahi kutetereka kusimama na chama chake tangu alipojiunga nacho na kuanza kushiriki siasa za mageuzi nchini.

Kwa niaba ya CHADEMA na wanachama wetu nchi nzima, napenda kutoa salaam za pole sana kwa familia ya marehemu, mjane na watoto. Natoa pole kwa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wanachama wa chama hicho, pia tunatoa pole kwa Jaji Mstaafu Joseph Warioba na makamishna wote wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwakifo cha Dkt. Mvungi. Tunaomba Mwenyezi Mungu awatie nguvu sana wakati huu wa majaribu na majonzi makubwa.

Dkt. Mvungi alikuwa mwanasiasa mwenye misimamo ambaye hakuwahi kukihama chama chake tangu alipoanza siasa za mageuzi nchini. Ni kati ya wasomi wachache waliokuwa na ujasiri na kuthubutu kujiunga na vyama vya upinzani tangu mapema.

"Mvungi pia alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa kupigania nchi yetu iwe na Katiba Mpya, ili hatimaye siasa zetu, hususan demokrasia ya vyama vingi nchini iendeshwe kwa misingi iliyo imara, amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza;

Mwenyezi Mungu alimjalia marehemu akaweza kushiriki kutimiza ndoto hiyo baada ya kuteuliwa kuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Mpya, kazi ambayo ameifanya hadi siku alipokutwa na tukio lililosababisha mauti yake.

Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, amesisitiza kuwa kwa namna ambavyo Dkt. Mvungi alikuwa mstari wa mbele katika suala hilo, Tume ya Katiba Mpya inao wajibu wa kuthamini mchango wake katika hatua iliyofikia sasa ya mchakato huo nyeti hadi utakapofika mwisho.

Wakati tukimwombea marehemu kwa Mungu, alazwe mahali pema peponi, ni matumaini yetu kuwa serikali kupitia vyombo vyake itahakikisha kuwa wale wote waliohusika katika tukio la lililosababisha kukatisha uhai wa Dkt. Mvungi wanapatikana na kuchukuliwa hatua zote zinazostahili kisheria, amesema Mwenyekiti Mbowe.
 
Hii ni habari ya huzuni kwelikweli. Nimepata mshtuko mkubwa na dimbwi la huzuni kupata taarifa ya kufariki leo hii kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwanasheria Mahiri na Kiongozi wa NCCR-MAGEUZI Dr. Sengondo Mvungi. Nilipata nafasi na heshima ya pekee kushirikiana naye wakati wa sakata la Wanafunzi 29 wa Kitanzania waliotelekezwa na serikali ya Tanzania huko Ukraine. Dr. Mvungi alikuwa mstari wa mbele kujitokeza wazi pasi ya kujali jina lake na nafasi yake kuwasemea vijana wale na kutoa mchango wake kwa hali na mali katika kuwasaidia vijana wale. NI wakati huo ndipo nilipotambua kujitoa kwake katika kupigania mabadiliko ya kweli ya kisiasa nchini.

Familia yake imepata pigo kubwa leo na taifa vile vile. Natumia nafasi hii kutoa pole za dhati kwa familia yake, ndugu na jamaa pamoja na chama chake ambacho kimempoteza mmoja wa viongozi wake mahiri. Nawaombe wote faraja wakati huu wa majonzi makubwa na Mwenyezi Mungu amhurumie ndugu yetu na kumpa pumziko la milele. Amina.
 
RIP Dr. Mvungi. Mungu akulaze mahala pema peponi. Japo umeondoka kivuli chako kitaishi. Aliyekuondoa atakufuata soon japokuwa hatakuona. Naipa pole familia yako. Maisha yetu kwa sasa nchini ni kudra za Mwenyezi Mungu. Ni kwamba tupigwe, wengine wamepona lakini wewe umeondoka. Hao wezi watapotea kama wapigaji wa wengine walivyo potea. Pole sana.
 
Too sad.. RIP Dr. Mvungi. Tutakukumbuka kwa harakati za kuwataka watanzania kuwa huru zaidi katika nchi yao..
 
Back
Top Bottom