TANZIA: Dr. Carjetan K. Maganga (Mzee wa EF 100) AMETUTOKA

mhuri25

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
2,666
3,451
Kwa wale waliopita UDSM hasa toka SoED, CoNAS na wale wa CoSS& CoHU mzee wetu mkufunzi wetu Dr Cajetan K. Maganga Mzee wa EF 100 ametutoka hatunae tena. namkumbuka mzee huyu kwa jinsi alivyokuwa mwalimu mashuhuri sana katika Philosophy of Education na alivyokuwa simple sana wale wadau wa CAFE ONE hata Kama sio wa Education utakuwa unamfahamu kwa kumuona katika foleni ya MENU
FB_IMG_1554759497819.jpeg


Typed Using KIDOLE
 
Daah huyu dingi namjua japo nilikuwa upande mwingine kabisa tofauti na course zake,la Saba B ,ila cafteria tulikuwa pamoja naye kwenye RB



Resiti ini pisi.....
 
Dah huyu mzee nilikuwa namkubali sana Professa lakni alikuwa anatembea kwa miguu kutoka pale UDSM akielekea kwake...nahisi ndo yalikuwa mazoez yake maana hiyo tembea yake!!..umri ulikuwa umeenda sana R.I.P MZEE WA essence.
 
Babu, nakumbuka pale UDSM lkn babu hukutaka kutoka hata ofisin, babu ulipanga folen pamoja na wanafunzi ili ununue chakula anachokula mwanafunzi wa UDSM pale cafteria.....babu hukutaka kudrive bali ulitaka kupanda daladala.....nenda unakostahili babu...ni Mungu pekee ndiye ajuaye juu yako....mwanadamu hajui lolote....nakumbuka somo lako EF babu.......ulikuwa na mbwembwe......
 
Daaah alikuwa na office yake nyuma ya cafe one pale mara nyingi nilikuwa napishana nae pale

Sijawahi kumuona akipanda gari mara nyingi alikuwa akitembea kwa miguu

Story za vijiweni eti alinyimwa u professor na baba wa taifa kisa alikuwa anakosoa sera zake

Ila hayana umuhimu tena katutoka tayari naamini ni pigo kwa wana udsm na wanafunzi wake pia

Kifo ni ukumbusho na sio lolote zaidi ya kipimo kwetu, safari yetu ni moja hakuna anae jua siku yake

R.I.P Dr Maganga
 
Dah......inakuwa ngumu kuamini vile.....mzee ile namuona kwa mara ya kwanza....mie ndo nkaona aibu kwa alivochomekea.......ndo nkaambiwa ni kawaida yake.......namna alivokuwa anafundisha ilikuwa haichoshi kumsikiliza.......ama kweli kifo hakichagui.......nenda salama mzee Maganga.......umetangulia.....mbele yetu nyuma yako tunafuata........rest in peace mzee
 
Kwa wale waliopita UDSM hasa toka SoED, CoNAS na wale wa CoSS& CoHU mzee wetu mkufunzi wetu Dr Cajetan K. Maganga Mzee wa EF 100 ametutoka hatunae tena. namkumbuka mzee huyu kwa jinsi alivyokuwa mwalimu mashuhuri sana katika Philosophy of Education na alivyokuwa simple sana wale wadau wa CAFE ONE hata Kama sio wa Education utakuwa unamfahamu kwa kumuona katika foleni ya MENUView attachment 1066436

Typed Using KIDOLE
Pumzika kwa amani babu nikikumbuka enzi zile ulikuwa unanikubali sana kwenye presantation kunisikiliza,na karibu wadau woooote wa jf wamepita kwako watakutakia pumziko jema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom