TANZIA: Diwani wa Kimwani Kagera auawa kwa kushambuliwa na mapanga

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
TANZIA: Diwani wa Kimwani, Kagera, Faustine Muliga (CUF) ameuawa kwa kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

RPC Ollomi athibitisha

Kijana huyu anaitwa "Simon Shilage" ana umri wa miaka 22, Yeye kwa kushirikiana na mwenzie mmoja ambaye bado hajapatikana ndio waliomuua Diwani wa kata ya Kimwai huko Muleba Ndg.Faustine Muliga wa chama cha wananchi CUF.

Kijana huyu amekamatwa jioni ya jana na wananchi wa kijiji cha Kyota akijaribu kutoroka. Amekutwa na panga lenye damu alilotumia kumuua diwani Muliga. Alipohojiwa amekiri kwamba ni kweli yeye na mwenzie mmoja (hakumtaja jina) ndio waliomuua Mhe.Muliga kwa kumkata mapanga.

Amesema kazi hiyo walitumwa na aliyekua mgombea udiwani wa Kata hiyo kwa ticket ya CCM kwenye uchaguzi uliopita, ambaye alikua mpinzani wa Muliga lakini alishindwa kwenye uchaguzi.

Ameongeza kuwa Mgombea huyo aliwaahidi kiasi cha shilingi milioni 1.5 ikiwa watafanikiwa kumuua Muliga na aliwapa "advance" ya shilingi laki moja na nusu (150,000/=). Baada ya makubaliano hayo vijana hao walimvamia Muliga nyumbani kwake majira ya saa 2 usiku akiangalia "Taarifa ya Habari" ambapo walimkata mapanga maeneo mbalimbali mwilini mwake kabla ya kutokomea kusikojulikana.

Kijana huyu alikamatwa na wananchi wenye hasira kali ambao walitaka kumuua lakini akaokolewa na Polisi. Hata hivyo wananchi hao walifanikiwa kumkata sikio lake moja la kushoto kama anavyoonekana pichani.

Kwa sasa anashikiliwa kituo cha Polisi Muleba kwa upelelezi, kabla ya kupandishwa Mahakamani kujibu tuhuma za Mauaji.!View attachment 320781
 
Kwanini Kagera kuna matukio kama haya kila mara. Mwaka jana kulikuwa na matukio ya uchomaji wa makanisa na mauaji holela pia!
 
Kama ni Siasa MUNGU awalaani kwani tutaacha kugombea sasa tuwaachie wenye kung'ang'ania kama uongozi ni mali yao
 
Mwenyezi mungu ahiraze mahali pema pepon r.I.p diwani kweli kama ni siasa tatazid kuwarahani
 
Inasadikika aliyemuua ni aliyekuwa mpinzani wake wakati wa uchaguzi toka CCM ambaye nyumba yake kwa sasa inateketezwa na wananchi
 
Back
Top Bottom