TANZIA: Diwani Elia Shukia wa Kata ya Mwanhuzi na Katibu wa Mbunge Meatu afariki kwa ajali ya gari

Online Pastor

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,949
2,000
Wakuu,

Kwa taarifa za awali ni kuwa Mhe Elia Shukia amefariki leo kwa ajali ya gari maeneo ya Manyoni.

8B1B6BDF-46DE-433A-90B8-390519682ED7.jpeg

1A38A814-E521-4070-8E2D-C911D62EF966.jpeg

9029B6C1-A87A-4254-85D8-D1F6CDA349D2.jpeg

Mhe Elia ambaye pia ni katibu wa Mbunge wa jimbo la Meatu alikuwa akitokea mkoani Dodoma,akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Meatu,Mwenyekiti wa Halmashauri na Dereva la gari husika.

Aliethibitisha msiba huu ni Mhe Diwani Anthony Philip wa Kata ya Makao!

Mhe Diwani alikuwa ameongozana na DED wa wilaya Meatu,dereva bwana Juma Jengua na Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo mpaka muda huu dereva naye ameshafariki huku DED na Mwenyekiti wa Halmashauri wakiwa wamewahishwa hospitalini mjini Itigi.

Mhe Diwani na wenzie walikuwa wanatoka mjini Dodoma kuonana na Katibu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Kwa kumbukumbu hii ni ajali ya pili kutokea ndani ya mwezi mmoja ikihusisha viongozi wa kisiasa wa wilaya ya Meatu.

Ajali ya kwanza ilitokea mwezi uliopita ukihusisha msafara wa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa hapa wilayani Meatu.

Katika msafara huo walikufa madiwani wawili wa CCM,hivyo kwa ajali ya leo,Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Meatu tayari kimeshapoteza madiwani watatu.

More updates to come!
 

Joselela

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,791
2,000
Hizo ndio sehemu zenyewe zina historia za ajali ya mara kwa mara serikali inatakiwa waweke post za ukaguzi maeneo hayo na pia wafunge speed detectors pembezoni mwa barabara..

Lakini shida kubwa ya hizi post ni rushwa na kila mahala ni rushwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom