TANZIA: Chief Shagali Afariki dunia

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Chief Gilead shangali amefariki dunia leo asubuhi akiwa katika matibabu Nairobi kenya.Msiba huko nyumbani kwake machame moshi.poleni sana wafiwa,Rongare, Stella , Winnie , Kenedy, Diana, na wanafamilia wote.Bwana alitoa na bwana ametwaa.Rest in peace mangi shangali
 
Mangi Gilead Abdiel Shangali alikuwa ni mangi wa mwisho kabisa kuwa hai kule uchagani miongoni mwa walioteuliwa kuwa watawala wa jadi nyakati za ukoloni. Wengine wote walishafariki. Mangi Gilead (kama alivyojulikana sana wakati wa uhai wake) alitawazwa rasmi kuwa mangi wa Machame mwaka 1952 kwa pendekezo la baba yake Abdiel Shangali ambaye kwa wakati huo alikuwa ameteuliwa na wakoloni wa kizungu kuwa mangi mwitori wa Hai (mnamo mwaka 1946).

Mangi Gilead ambaye alitawazwa kuwa mangi akiwa kijana kabisa wa miaka ya ishirini, alikuwa ni miongoni mwa watawala wachache kabisa kuingia kwenye umangi wakati baba yake akiwa bado hai na kwa ridhaa yake. Hii ilimsaidia sana mwanzoni mwa utawala wake hasa kutokana na kuchukua madaraka kwenye utawala ambao ulikuwa mgumu zaidi kisiasa kule uchagani. Alitawala kwa miaka kumi tu kabla tawala za kijadi kufutwa kisheria nchini Tanganyika baada ya uhuru mwaka 1961. Anakumbukwa sana kwa upole wake, busara, na bidii yake ya kuhakikisha Machame inakuwa na shule za kutosha na maendeleo yaliyofanywa na tawala za nyuma yake yanadumishwa na kuboreshwa zaidi.

Hata hivyo hakuwa mtawala mwenye haiba na mshawasha ambao wamachame wengi walizoea katika tawala za nyuma. Alionekana kutokuwa na msukumo sana kisiasa, asiyeshiriki kwenye mabadiliko mbalimbali ya kijamii Machame na hata uchagani, na mchango wake wa kuhakikisha Machame inaendelea kuwa kinara wa mabadiliko ya kijamii ulituhumiwa kuwa mdogo sana. Alionekana kupwaya kisiasa na kuwa tofauti sana na baba yake mdogo, mangi Charles Shangali wa Masama ambaye aliendelea kuwa na mguso wa kisiasa, kimila, na kwenye maendeleo ya jamii hata baada ya umangi kufutwa.

Pamoja na baba yake walisaidia sana TANU kuwa na misingi ya kisiasa kule uchagani hasa kutokana na watawala wengine kuwa na shaka na siasa za TANU. Hata hivyo, baada ya umangi kufutwa hakupenda sana kujihusisha moja kwa moja na siasa zenye mirengo ya vyama vya siasa huku akipendelea zaidi shughuli zake binafsi. Kitendo cha CHADEMA kuonekana kuisumbua sana CCM Hai inawezekana kutafsiriwa na baadhi ya wana CCM wa mrengo wa kulia kwamba hajatumia nafasi yake vya kutosha kuitetea CCM, hasa Machame. Lakini mtazamo huu si sawasawa kabisa. Watawala wa Machame siku zote wamekuwa ni viongozi wa watu wote na wasio na mirengo ya baadhi ya watu fulani kwenye jamii yao. Mangi wa Machame alikula yamini kuitumikia jamii yake yote na ikibidi kufa kwa ajili ya kuitetea jamii yake. Alitakiwa kuwajali na kuwathamini wamachame wote, na kudhani kwamba atakishabikia chama fulani dhidi ya vingine ni kupotea njia. Kwa hiyo inaonekana aliamua kuishi kwa jinsi ya kiapo chake alichokula na kufuata nyayo za babu zake walioshiriki kujenga, kuimarisha, na kulinda siasa za Machame na hatimaye uchagani kwa miaka zaidi ya 300.
 
Kwanini unatukumbusha Ufoo Saro, mbona tumeanza kusahau?
RIP CHIEF SHANGALI.

cc. Smile.
 
Last edited by a moderator:

Mohamed Said akisoma habari hii anaweza kuangauka kwa uchungu. Huyo na baba yake hawamo katika kundi la kidongo chekundu na Gerezani ati!

RIP Mangi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom