TANZIA TANZIA: Balozi Augustine Philip Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amefariki dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,795
11,958
4FEBC882-5C8B-4461-B946-C86759C3DF06.png


Rais Magufuli anatangaza kifo cha Waziri wake wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga aliyefariki leo alfajiri Mei 01, Jijini Dodoma

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema Waziri huyo aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake na alifikishwa hospitalini akiwa tayari ameshafariki dunia

IMG_20200501_075258.jpg


WASIFU:

Augustine_Mahiga.jpg


Dk Augustine Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945 huko Tosamanganga, Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa (atatimiza miaka 70 ifikapo Agosti mwaka huu). Amesoma elimu ya msingi katika shule za Serikali enzi ya mkoloni na alihitimu darasa la VIII muda mfupi baada ya uhuru. Safari ya elimu ya Dk Mahiga ilikuwa ya umaskini uliopitiliza, alishindwa kuendelea na elimu ya sekondari kwa kutokuwa na fedha za kulipia mashuka na mablanketi hadi aliposaidiwa na msamaria mwema kutoka Shirika la Kennedy wakati huo.

Aliendelea na masomo ya sekondari hapahapa nchini na mwaka 1968, alijiunga katika Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam na kuhitimu Shahada ya Sanaa akibobea kwenye elimu mwaka 1971.

Mwaka huohuo, Dk Mahiga alipata ufadhili na kuendelea na masomo ya juu nchini Canada katika Chuo Kikuu cha Toronto ambako alihitimu Shahada ya Uzamili. Aliendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katika chuo hichohicho akijikita katika Uhusiano wa Kimataifa na kuhitimu mwaka 1975.

Mwaka huohuo 1975 (akiwa na miaka 30), Dk Mahiga alirejea nchini akiwa daktari wa falsafa kitaaluma na alipangiwa kazi ya kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa mhadhiri katika Idara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kikanda. Alifanya kazi hiyo hadi mwaka 1977 alipohamishiwa katika Ofisi ya Rais kuwa Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo na alidumu hapo akifanya kazi pamoja na Mwalimu Julius Nyerere hadi mwaka 1980.

Kati ya mwaka 1980 hadi 1983, Dk Mahiga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Nafasi hii aliitumikia kwa weledi mkubwa katika historia ya watu waliowahi kuitumikia, aliweza kuifahamu nchi vizuri na mifumo yake kwa mtizamo wa ndani na nje.

Mwaka 1989 hadi 1992, aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Kimataifa akifanyia kazi Geneva, Uswisi na mwaka 1992 hadi 1994, Balozi Mahiga aliteuliwa kuwa Kiongozi (Mwakilishi) wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi duniani (UNHCR) mjini Monrovia, Liberia na huu ndiyo wakati aliponusurika kuuawa na Majeshi ya Rais Charles Taylor, kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe. Kuna wakati akiwa katikati ya operesheni ya wakimbizi hapo Monrovia, Serikali ya Tanzania ilimteua kuwa Balozi na kumuongezea jukumu jingine zito.

Mwaka 1994 -1998, Balozi Mahiga alihudumu akiwa Mratibu na Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni ya Dharura ya Ukanda wa Maziwa Makuu akifanyia kazi hiyo kutokea Geneva, Uswisi na kati ya mwaka 1998 - 2002 aliteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu (Mwakilishi) wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) huko mjini Delhi India kabla ya kuteuliwa tena kuwa mwakilishi wa shirika hilo katika nchi za Italia, Malta na Jamhuri ya San Marino kati ya mwaka 2002 - 2003.

Balozi Mahiga amepata pia kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2010 na alishiriki kikamilifu katika mipango ya kimataifa pamoja na kusimamia mazungumzo ya kuanzishwa kwa Kamisheni ya Ujenzi wa Amani (mwaka 2005). Pia kushiriki kwenye masuala ya maingiliano ya serikali mbalimbali na makundi yanayofanya kazi zisizo rasmi, maendeleo, amani, usalama na ujenzi wa ushirikiano wa uhakika kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Balozi Mahiga alirejesha heshima ya Tanzania hadi kuwa mojawapo ya nchi zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi yetu ilipopata heshima hiyo, yeye aliteuliwa kuwa mkuu wa ujumbe wa Tanzania katika Baraza hilo, hii ilikuwa ni mwaka 2005.

Mwaka 2015 mwezi Disemba, Rais Magufuli alimteua Balozi Mahiga kuwa Mbunge na baadae kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Naibu wake akiwa Dr Suzan Kolimba.

Machi 03, 2019 Rais Magufuli alimhamisha Wizara na kumteua kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, nafasi aliyoitumikia hadi mauti yanamkuta.


MACHACHE KUHUSU DKT. MAHIGA: Augustine Mahiga: Mwanadiplomasi anayeheshimiwa kuliko wote Tanzania - JamiiForums

MAZISHI: Mazishi ya Dkt. Augustine Philip Mahiga kijijini kwake Tosamaganga mkoani Iringa. Mkewe ashindwa kuhudhuria baada ya kuwa Kenya akiuguza mtoto - JamiiForums
 
R.I.P Mahiga

Ama kwa Hakika Taifa limepoteza mtu makini na mwerevu.

Sasa ni wakati kwa Serikali itambue kwamba viongozi wa Juu ambao tunaamini wao ndio wapo katika nafasi nzuri ya kupata matibabu na kinga wanapopoteza maisha wakati huu huku Serikali kutoonesha nia ya dhati kupambana na hili Janga basi huu ni Ujumbe tosha kwa Dunia kwamba Mamlaka zimeshindwa kulinda watu wake na hivyo Nchi haipo salama sasa hivi na siku zijazo hata majanga mengine yatakapotokea.
 
Hii corona naona imeingia Ikulu live mchana kweupe.
Ifike wakati viongozi wa Tanzania wajifunze kujiuzuru pale ushauri wao unapopuuzwa.

Waziri Mkuu na Waziri wa afya ilibidi wawe wamejiuzulu toka siku nyingi.

Sidhani kama msimamo wa Rais ndio msimamo wao, hawana namna sababu ya kulinda vibarua vyao.

Uhai ndio kila kitu hivyo vyeo mnakufa mnaviacha, kama kiongozi mkubwa hataki kufuata ushauri wa wataalamu ni kumwachia serikali aongoze peke yake.
 
Aisee. Apumzike kwa amani mzee.

Mazishi yake yatakua ya watu 10 tu?

Hii kitu ikipiga juu ndio labda watachukua hatua. Mshikaji kakimbilia kijijini kwao huku wenzake wanateketea. Yule kumuona mjini labda mwezi wa 8.

Uzuri wa hii kitu ndio huo, na vile wakubwa wengi ni wazee na most volnerable and prime suspect ya hii kitu, ikiwaanza wataisha. Labda hii itasababisha tuchukue hatua madhubuti ingawa tumechelewa tayari.
 
Back
Top Bottom