TANZIA: Amri Athuman (King Majuto) afariki dunia akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili

Kylian D

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
206
357
TANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.

Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''

E6EBFA7D-C906-4ACF-970B-1EF150AA1393.jpeg

MAJUTO22.jpg

km5.jpg

Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.

Pia soma >
Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
Mzee Majuto atangaza rasmi kuacha kuigiza, sasa kumrudia Mungu wake
Mwakyembe Kuivaa kampuni iliyomdhurumu Mil 25 Mzee Majuto.
Haya ndio maisha halisi anayoishi mzee Majuto
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji, mwandishi wa mswada.

Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company (TFC). King Majuto alikuwa ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
 
MAISHA HAYA WAKATI MWINGINE UKIFIKIRIA: HAKUNA HAJA YA KUGOMBANA NI KUJIWEKEA UADUI, CHUKI na watu n.k kwa MAANA sote tutapita, Mali na DUNIA ITABAKI!
Ni heri kuishi kwa upendo ili kuacha legacy nzuri kwa watu kama huyu mzee! Mungu ampokee! Amina.
Screenshot_20180808-210345.png
 

Similar Discussions

46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom