TTANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu.
Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.
“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''
View attachment 830443Pia soma >
View attachment 830484
View attachment 830455
Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli waliopokwenda kumjulia hali King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.
Mzee Majuto: Tanzanian Movie and Comedy Legend
Mzee Majuto atangaza rasmi kuacha kuigiza, sasa kumrudia Mungu wake
Mwakyembe Kuivaa kampuni iliyomdhurumu Mil 25 Mzee Majuto.
Haya ndio maisha halisi anayoishi mzee Majuto
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.
Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.
Mimi mwenyewe nimeshangaa kila nikiingia nauwona juu leo nikaona niingie kunani watu wana reply kilasiku auMods wa Jf;
Hivi ni kwa nini mpaka leo huu uzi umewekwa kipaumbele kila ukifungua hili Jukwaa unakutana nao?
Sent using Jamii Forums mobile app
Umewekwa kipaumbele kwa sababu ni gwiji wa tasnia ya vichekesho,Mimi mwenyewe nimeshangaa kila nikiingia nauwona juu leo nikaona niingie kunani watu wana reply kilasiku au
Portfolio | 2020
Angalia tarehe za uzii