TANZIA Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya tatu, Iddi Mohamed Simba afariki dunia

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya tatu, Iddi Mohamed Simba amefariki dunia leo.

Taarifa zilizothibitishwa na mtoto wake, Sauda Simba Kilumanga zinasema Iddi Simba amefariki katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mungu amlaze mahali pema peponi

1.jpg
Iddi Simba amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, akiishi London Uingereza kati ya mwaka 1978 na 1981 na kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki kati ya mwaka 1968 na 1978 makao makuu Uganda.

Kabla ya kujiuzulu, Simba alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara (1997 hadi 2001. Mwaka 2003 Iddi Simba aliandika kitabu alichokiita 'Dhana ya Uzawa'.

Aliwahi kuwa mbunge wa jimboni la Ilala takriban kwa miaka 10.
 
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya awamu ya tatu, Idd Simba amefariki dunia leo.

Taarifa zilizothibitishwa na mtoto wake Sauda Simba Kilumanga zinasema Idd Simba amefariki katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu.

IMG_20200213_121517_303.jpeg
 
Back
Top Bottom