TANZIA Aliyewahi kuwa Waziri na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omary Nundu amefariki dunia

babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,643
3,287
index.jpg

Waziri wa zamani nchini Tanzania, Omary Nundu amefariki dunia na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imethibitisha.

Omari R Nundu, alikuwa mwanachama wa JamiiForums tangu Novemba 2007.

Mnamo tarehe 27 February 2017 Rais Magufuli alimteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL.

Nundu aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga kuanzia mwaka 2010 hadi 2015

******

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Dk Omary Nundu (71) amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa leo mchana Jumatano Septemba 11, 2019 na Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam kimesema, “Waziri wa zamani Omary Nundu alifikishwa leo MNH, akitokea nyumbani kwa gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.”

“Hivyo waliomleta waliamua wakahifadhi mwili wake katika hospitali ya rufaa ya Jeshi Lugalo,” imeeleza taarifa hiyo
Dk Nundu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mbunge wa Tanga na Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya awamu ya nne ya Tanzania.

Juni 12, 2019, Rais wa Tanzania, John Magufuli alimteua Dk Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International.

Katika makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania pamoja na ofisa mkuu wa ufundi wanapaswa kuteuliwa na Serikali.

Historia Ya Marehemu, Omary Nundu

Omari Rashid Nundu, alizaliwa Tanga, Tanzania mwaka 1948 na huko ndiko alikopata elimu yake ya shule kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland mwaka 1971 kusomea uhandisi na sayansi ya vyombo vya anga (Aeronautical Engineering); na baadaye kuendelea na shahada za juu na utafiti vyuo vikuu vya Cranfield, England na Concordia, Canada.

Omari amebahatika kufanya kazi kwenye taasisi mbalimbali duniani katika kuitendea haki taaluma hiyo aliyoisomea na anayoipenda. Kwa nyakati mbalimbali alikuwa mhandisi na mkurugenzi kwenye mashirika ya ndege, alikuwa mshauri na mhadhiri kwenye vyuo vya kimataifa, na pia alikuwa mkuu wa vitengo vya usafiri wa anga katika jumuia za kimataifa.

Kabla ya kurejea Tanzania na kuwa mbunge wa Tanga na pia Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa Rais wa jopo la kimataifa la magwiji wa taaluma ya Usafiri wa Anga Duniani (Air Navigation Commission) kwa miaka miwili mfululizo

Ingawa ni mhandisi na mwana sayansi aliyebobea, Omari anapenda kuongea lugha mbalimbali lakini ana mapenzi ya dhati kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyomkuza. Hivyo basi kuwa yeye ni malenga wa mashairi halishangazi. Utenzi uliomo mwenye kitabu hiki unajaribu kusimulia maisha na mwenendo wa Dunia kwa kadri alivyoyashuhudia mhandisi huyu hadi mwaka 2015.
 
Duh, Pumziko La Amani apate Mzee.

Alikuwa anapiga shughuli gani baada ya kuacha ubunge?
 
Omari-Nundu-akifafanua.jpg

Waziri wa zamani nchini Tanzania, Omary Nundu amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hospitali hiyo imethibitisha.

> Mnamo tarehe 27 February 2017 Rais Magufuli alimteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL.

> Nundu aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga kuanzia mwaka 2010 hadi 2015
*******

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Dk Omary Nundu (71) amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa leo mchana Jumatano Septemba 11, 2019 na Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam kimesema, “Waziri wa zamani Omary Nundu alifikishwa leo MNH, akitokea nyumbani kwa gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.”

“Hivyo waliomleta waliamua wakahifadhi mwili wake katika hospitali ya rufaa ya Jeshi Lugalo,” imeeleza taarifa hiyo
Dk Nundu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mbunge wa Tanga na Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya awamu ya nne ya Tanzania.

Juni 12, 2019, Rais wa Tanzania, John Magufuli alimteua Dk Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International.

Katika makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania pamoja na ofisa mkuu wa ufundi wanapaswa kuteuliwa na Serikali.

Historia Ya Marehemu, Omary Nundu

Omari Rashid Nundu, alizaliwa Tanga, Tanzania mwaka 1948 na huko ndiko alikopata elimu yake ya shule kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland mwaka 1971 kusomea uhandisi na sayansi ya vyombo vya anga (Aeronautical Engineering); na baadaye kuendelea na shahada za juu na utafiti vyuo vikuu vya Cranfield, England na Concordia, Canada.

Omari amebahatika kufanya kazi kwenye taasisi mbalimbali duniani katika kuitendea haki taaluma hiyo aliyoisomea na anayoipenda. Kwa nyakati mbalimbali alikuwa mhandisi na mkurugenzi kwenye mashirika ya ndege, alikuwa mshauri na mhadhiri kwenye vyuo vya kimataifa, na pia alikuwa mkuu wa vitengo vya usafiri wa anga katika jumuia za kimataifa.

Kabla ya kurejea Tanzania na kuwa mbunge wa Tanga na pia Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa Rais wa jopo la kimataifa la magwiji wa taaluma ya Usafiri wa Anga Duniani (Air Navigation Commission) kwa miaka miwili mfululizo

Ingawa ni mhandisi na mwana sayansi aliyebobea, Omari anapenda kuongea lugha mbalimbali lakini ana mapenzi ya dhati kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyomkuza. Hivyo basi kuwa yeye ni malenga wa mashairi halishangazi. Utenzi uliomo mwenye kitabu hiki unajaribu kusimulia maisha na mwenendo wa Dunia kwa kadri alivyoyashuhudia mhandisi huyu hadi mwaka 2015.
 
Huyu ndie aliyetudanganya na kutuaaminisha kuwa Airtel ni mali ya Serikali kumbe muongo mkubwa. Walikuja wahindi wenye kampuni yao, sijui porojo zake ziliishia wapi?
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom