TANZIA: Aliyewahi kuwa Waziri na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omary Nundu amefariki dunia

babumapunda

babumapunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
4,308
Points
2,000
babumapunda

babumapunda

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
4,308 2,000
index-jpg.1204522

Waziri wa zamani nchini Tanzania, Omary Nundu amefariki dunia na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imethibitisha.

> Omari R Nundu, alikuwa mwanachama wa JamiiForums tangu Novemba 2007.

> Mnamo tarehe 27 February 2017 Rais Magufuli alimteua Omary Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL.

> Nundu aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga kuanzia mwaka 2010 hadi 2015

******

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Dk Omary Nundu (71) amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa leo mchana Jumatano Septemba 11, 2019 na Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam kimesema, “Waziri wa zamani Omary Nundu alifikishwa leo MNH, akitokea nyumbani kwa gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.”

“Hivyo waliomleta waliamua wakahifadhi mwili wake katika hospitali ya rufaa ya Jeshi Lugalo,” imeeleza taarifa hiyo
Dk Nundu enzi za uhai wake aliwahi kuwa mbunge wa Tanga na Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya awamu ya nne ya Tanzania.

Juni 12, 2019, Rais wa Tanzania, John Magufuli alimteua Dk Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International.

Katika makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania pamoja na ofisa mkuu wa ufundi wanapaswa kuteuliwa na Serikali.

Historia Ya Marehemu, Omary Nundu

Omari Rashid Nundu, alizaliwa Tanga, Tanzania mwaka 1948 na huko ndiko alikopata elimu yake ya shule kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland mwaka 1971 kusomea uhandisi na sayansi ya vyombo vya anga (Aeronautical Engineering); na baadaye kuendelea na shahada za juu na utafiti vyuo vikuu vya Cranfield, England na Concordia, Canada.

Omari amebahatika kufanya kazi kwenye taasisi mbalimbali duniani katika kuitendea haki taaluma hiyo aliyoisomea na anayoipenda. Kwa nyakati mbalimbali alikuwa mhandisi na mkurugenzi kwenye mashirika ya ndege, alikuwa mshauri na mhadhiri kwenye vyuo vya kimataifa, na pia alikuwa mkuu wa vitengo vya usafiri wa anga katika jumuia za kimataifa.

Kabla ya kurejea Tanzania na kuwa mbunge wa Tanga na pia Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa Rais wa jopo la kimataifa la magwiji wa taaluma ya Usafiri wa Anga Duniani (Air Navigation Commission) kwa miaka miwili mfululizo

Ingawa ni mhandisi na mwana sayansi aliyebobea, Omari anapenda kuongea lugha mbalimbali lakini ana mapenzi ya dhati kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyomkuza. Hivyo basi kuwa yeye ni malenga wa mashairi halishangazi. Utenzi uliomo mwenye kitabu hiki unajaribu kusimulia maisha na mwenendo wa Dunia kwa kadri alivyoyashuhudia mhandisi huyu hadi mwaka 2015.
 
PROF NDUMILAKUWILI

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Messages
8,931
Points
2,000
PROF NDUMILAKUWILI

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2016
8,931 2,000
Pole kwa wafiwa.

Nini kimepelekea mauti yake???
 
PROF NDUMILAKUWILI

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Messages
8,931
Points
2,000
PROF NDUMILAKUWILI

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2016
8,931 2,000
Pole kwa wafiwa.

Nini kimepelekea mauti yake????
 
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Messages
2,260
Points
2,000
Alvajumaa

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2018
2,260 2,000
Innalillah wainnailillah raijuun
 
cmp

cmp

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
3,294
Points
2,000
cmp

cmp

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
3,294 2,000
Inawezekana kweli kulikuwa upigaji hela za matibabu ya nje lakini si vizuri kusema Watanzania wote watatibiwa hapa hapa. Hili wimbi la viongozi au wake wa viongozi kufariki mikononi mwa madaktari wetu limekuwa kubwa.

Hivi kweli huyu Dr Harrison Mwakyembe na Prof Mwandosya wangekuwa wameugua kipindi hiki cha Meko wangepona na kurejea kwwnye afya walizonazo leo kwa huduma za MNH? Last month mke wa AG Killangi alikufa pia.

Ikibidi kiongozi aende nje kwa matibabu nashauri aende tu, ila kama kuna mtu anataka kupiga hela, adhibitiwe mbona mifumo ipo.
Huko nje hawafi?
 
M

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2011
Messages
5,361
Points
2,000
M

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2011
5,361 2,000
Inalilah waina ilayhi Rajiuun
 
mtima nyongo

mtima nyongo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Messages
1,831
Points
2,000
mtima nyongo

mtima nyongo

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2015
1,831 2,000
nisiwe mnafiki,hawa watu wa kijani wafe tu tena wafe,hawa ndio bungeni kazi yao huwa ni ndiooooo na kupiga vigelegele.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,578
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,578 2,000
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani na awape faraja wafiwa wote katika wakati huu mgumu na wa majonzi. Amina
 
Hajto

Hajto

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Messages
2,993
Points
2,000
Hajto

Hajto

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2013
2,993 2,000
Duniani tunapita tu!!
Ni kweli kabisa tunapita,ila wale wanaojifanyaga sana kuwadhulumu na kuwatesa wenzao kwahilo basi wakumbuke kuwa hapa duniani tunapita,maamuzi wanayopewa na viongozi wao hayatawasaidia siku ya kufa na katika kaburi utakalolazwa,Jamani tuishini kwa adabu na heshima katika hii dunia
 
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
485
Points
500
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
485 500
Kwahyo umekoment usichokijua (pitia huo Uzi wote.unakela
 
mbenge

mbenge

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2019
Messages
205
Points
500
mbenge

mbenge

JF-Expert Member
Joined May 15, 2019
205 500
RIP Nundu, may your soul rest in peace. Amen.
 
Hercule Poirot

Hercule Poirot

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
1,449
Points
2,000
Hercule Poirot

Hercule Poirot

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
1,449 2,000
Apumzike kwa Amani.
Sie sote ni wa njia moja
 

Forum statistics

Threads 1,336,678
Members 512,696
Posts 32,547,530
Top