TANZIA Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou, afariki dunia

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
kabu.jpg
Aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma mjini Dkt. Amani Walid Kabourou, ametangulia mbele ya haki.

Alikuwa kalazwa Hospitali ya Muhimbili. Mazishi yanafanyika Kigamboni Dar Es Salaam.

Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Ameni.

KWA UFUPI:

Marehemu alizaliwa 23 Mei, 1949.

Aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia CCM mnamo mwezi Septemba 2006 na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma mwezi Oktoba mwaka 2012.

Aliwahi kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki kuanzia 05 Juni, 2007 hadi 04 Juni, 2012

UPDATE.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi
c916615902a3bcbbc9f5074b892388c8.jpg


More Updates
CHADEMA watoa salamu za rambirambi

CHADEMA.jpg
 
Aliyekuwa mbunge wa Kigoma mjini Dkt. Amani Walid Kabourou, ametangulia mbele ya haki.

Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Ameni.



Mbunge wa Kigoma mjini ni Mh.Zitto Kabwe na yupo hai akiendelea kutimiza majukumu yake,kusema "aliyekuwa" si sahihi,ilipaswa isomeke"aliyewahi kuwa".

By the way, Kifo cha mwanaCCM yeyote yule hakinihusu, siwezi kuuvika moyo wangu simanzi kwa kuomboleza vifo vya wauwaji,watesaji na watekaji,muda huo sina.

Mungu amlipe sawa sawa na matendo yake, Amen.
 
Ingefaa zaidi azikwe Kigoma kwa kuwa kule ana historia kubwa na ndefu!!
RIP
 
Pumzika kwa amani Daktari Amani Walid Kabourou.

Daima utakumbukwa kwa kuhamia Chadema kinyemela kutoka NCCR-Mageuzi (1993), kisha baadaye kuhamia CCM.
 
Back
Top Bottom