Tanzia: Aliyewahi kuwa Jaji Mkuu Zanzibar, Mzee Ali Haji Pandu afariki Dunia

27 Apr 2020
Zanzibar , Tanzania

Ex- Chief Justice Ali Haji Pandu RIP

Mzee Ali Haji Pandu, mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar, alifariki Jumatatu ya tarehe 27 Aprili 2020 Mjini Unguja na kuzikwa kwao Makunduchi.

Hapa mmoja wa watu waliomjuwa kwa karibu, Ismail Jussa, anasimulia wasifu wake:
  • Kuzaliwa 1938
  • Masomo Skuli ya Makunduchi
  • Masomo Skuli sekondari Ben Bella
  • Skuli ya Lumumba (King George the VI)
  • Scholarship nchini Yugoslavia, Belgrade University shahada mbili za sheria 1962
  • Sheha / Murdir (wilaya ya Chakwa) Peoples Court Wilaya ya Kati 1962 - 1964
  • Mtumishi wa Mahakama 1964 - 1970
  • Jaji Mkuu Mahakama Znz 1970-1978
  • 1978 ajiuzulu Ujaji Mkuu wa Zanzibar kutokana na kutoridhika na jinsi kesi ya uhaini ilivyoendeshwa Kesi Katika Mahakama Bandia ya Zanzibar – Tishio la Ukombozi
  • 1978 aligombea ubunge akashindwa
  • 1980 akagombea tena na hakufanikiwa
  • 1980 Mrajisi Mkuu wa serikali SMZ mambo msingi mpaka mwaka1984
  • 1985 Mwakilishi (mbunge) Baraza la Wakilishi Zanzibar wa CCM jimbo la Makunduchi
  • Waziri wa SMZ Ardhi Majenzi Maji 1985
  • Waziri SMZ Maliasili bahari misitu 1985
  • 1988 Mzee Pandu, Maalim Seif na wenziwe kadhaa kufukuzwa uanachama CCM kutokana na kilichoitwa 'Kuchafuka kwa hali ya hewa' ya kisiasa Zanzibar Masimulizi ya Thabiti Kombo kuhusu kuchafuka kwa hali ya hewa kisiasa
  • Kuwekwa kizuizini 1990 chini ya amri ya rais kwa miezi sita Document
  • KAMAHURU 1990 Shaaban Mloo
  • Kuunganisha Civic United na KAMAHURU Member : Civic United Front (CUF)
  • CUF 1992
  • ACT Wazalendo 2019


Source : Weyani TV
 
27 Apr 2020
Unguja, Zanzibar

JAJI MKUU WA KWANZA MZALENDO WA ZANZIBAR MZEE ALI HAJI PANDU AMEFARIKI DUNIA

Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Makungu alikuwa miongoni mwa viongozi wengi waliohudhuria mazishi ya mwendazake marehemu jaji Ali Haji Pandu ambaye ameacha watoto 9 na kizuka.


Source : ZBC Zanzibar
 
Back
Top Bottom