Jioni ya Oktoba 24 mwaka 2004, pale Old Trafford katika pambano la ligi kuu ya Uingereza, Man Utd Vs Arsenal, Jose Antonio Reyes akiwa ameanza upande wa kushoto alikuwa anakabwa na muingereza mfia timu, mzaliwa wa jijini Manchester, Gary Neville.
Gary Neville alitumia muda wake mwingi wa mchezo akimchapa viatu Jose Antonio Reyes huku mwamuzi Mike Riley "Kibichwa" akifumba macho na kujifanya haoni kinachoendelea huku Gary Neville akiambulia tu kadi ya manjano mpaka pale Reyes alipotolewa kipindi cha pili na kupelekea Arsenal kupokea kipigo cha 2-0 na kufanya kuhitimisha mechi 49 bila kufungwa kwenye EPL na pambano hilo likabatizwa jina la Battle of the Buffet.
Huyo ndio Jose Antonio Reyes, mshambuliaji aliyekuwa na utulivu wa hali ya juu, control ya kuvutia pia jicho la pasi kwa wenzake. Kumzuia Reyes kuna muda ulihitaji umchezee sana rafu ili asilete madhara golini mwako.
Asante kwa kumbukumbu nzuri sana Reyes, tangulia kapumzike kwa amani, nyakati ngumu hazipiti ila watu wagumu wanapita.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.